1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mo Ibrahim: Maendeleo kuhusu utawala bora Afrika yakwama

23 Oktoba 2024

Ripoti ya Wakfu wa Mo Ibrahim iliyochapishwa leo Jumatano imesema kuwa maendeleo kuhusu utawala barani Afrika yamesimama wakati ambapo haki za usalama na kisiasa zimedorora katika mataifa mengi.

Mo Ibrahim | Mjasiriamali wa simu za mkononi wa Uingereza-Sudan
Mwanzilishi na Mwenyekiti wa Wakfu wa Mo Ibrahim, Mo Ibrahim, akizungumza wakati wa mahojiano na AFP ofisini kwake London Novemba 16, 2020.Picha: Hollie Adams/AFP/Getty Images

Akiizungumzia ripoti hiyo muasisi wa taasisi hiyo Mo Ibrahim amesema Afrika ilipiga hatua kubwa katika miongo ya nyuma lakini katika miaka kumi iliyopita bara hilo limekuwa likijikokota. Ibrahim, mwenye umri wa miaka 78, ameongeza kwamba hali si nzuri na kuwa katika miaka mitano iliyopita maendeleo katika utawala yameanza kukwama na hata kurudi nyuma katika baadhi ya mazingira. Kulingana na ripoti ya taasisi yake, hali inaonekana kuwa afadhali kwa visiwa vya Shelisheli ambavyo vimeshika nafasi ya kwanza katika faharasa hiyo. Masuala kadhaa yameonekana pia kuboreshwa kote Afrika ikiwemo miundombinu, usawa kwa wanawake pamoja na afya na elimu. Maboresho hayo hata hivyo, yanadhoofishwa na kuporomoka kwa utawala wa sheria, haki, ushiriki wa kisiasa na hasa usalama. Faharasa ya wakfu wake inayochapishwa kila baada ya miaka miwili, inazingatiwa kuwa utafiti wa kina zaidi, ikikusanya data kwa vigezo 322 vikiwemo huduma za umma, haki, ufisadi na usalama.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW