Mafaniko au ahadi tupu tokea kupitishwa kwa azimio la haki za binadaamu miaka 60 iliopita
1 Desemba 2008Je kuna sababu ya kusheherekea kwa kuzingatia hali mbaya ilioko duniani ya kutotimizwa kwa ahadi za azimio hilo.Ulrike Mast- Kirschning wa Deutsche Welle anapitia matokeo ya hali hiyo.
Nini jibu la jinamizi la uvunjaji mkuu wa haki za binaadamu na mataifa ya kiimla katika karne ya 20.Nini jibu la vita vya pili vya dunia na utawala wa kinyama wa Ujamaa wa kitaifa wa Ujerumani na mauaji ya kimbari ya Wayahudi barani Ulaya.
Ilikuwa ni hatua ya kihistoria kwa hali ya haki za binaadamu kwa kuwa na kitu kipya kidogo amesema hayo Eleanor Roosevelt katika kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini Paris Ufaransa hapo mwaka 1948.Kwa mara ya kwanza kabisa mataifa duniani yameanzisha sheria ya mfumo wa thamani kwa binaadamu wote.
Baraza hilo kuu la Umoja wa Mataifa lilitangaza vifungu 30 hasa juu ya haki za uhuru wa binadaamu,haki za kiuchumi, kijamii na kitamaduni.Mwanzoni ilikuwa hulazimiki kuzitekeleza kisheria na hadi hii leo kwa kiasi kikubwa kile kinachojulikana kama haki za kiraia zimekuwa zikiendelea kukandamizwa.Heiner Bielefeldt mkuu wa taasisi ya haki za binaadamu nchini Ujerumani anasema kuna tafauti kubwa kati ya kutimiza wajibu huo na ukweli wa mambo .
Kwa muda wote mkutano wa Umoja wa Mataifa wa haki za binaadamu mjini Vienna hapo mwaka 1993 ulijadili suala hilo.Masuala mbali mbali ya haki za binaadamu yaliibuka katika mkutano huo.
Baraza la haki za binaadamu ambalo ni jopo la kisiasa kwa siasa za haki za binaadamu za Umoja wa Mataifa pia ni changamoto kwa siasa za nje za Ujerumani kama alivyosema hapa waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank Walter Steinmeir.
Amesema walikuwa tanajuwa ugumu wa kuanzishwa kwake na walikuwa wakweli wakati waliposema kwamba wanaweza na wanapaswa kujitahidi zaidi na kwa ufanisi.Daima imekuwa ni fikra yao kwamba Baraza hilo la Haki za Binaadamu ni madhubuti zaidi kuliko ilivyokuwa Tume ya Haki za Binaadamu lakini iwapo litakuwa imara kiasi gani bado kupangwa lakini wamekubaliana kulifanyia kazi zaidi.
Wakati Umoja wa Mataifa ukiadhimisha miaka 60 ya kutangazwa kwa Azimio la Haki za Binaadamu suala la kujiuliza ni iwapo kuna mafanikio au ni ahadi tupu.