Mafuriko Indonesia, Sri Lanka: idadi ya vifo yafika 1,000
1 Desemba 2025
Matangazo
Maeneo ya baraAsia yanakumbwa na mafuriko mabaya ambayo yamesababisha maafa makubwa ikiwemo vifo.
Sri Lanka na Indonesia ndizo nchi ambazo zimeathiriwa zaidi, na zimepeleka wanajeshi kuwasaidia manusura.
Mafuriko hayo yamesababishwa na mvua kubwa iliyonyesha kwa muda mrefu wiki iliyopita kote katika kisiwa cha Sri Lanka na katika maeneo mengi ya kusini mwa Thailand na kaskazini mwa Malaysia.
Idadi hiyo ya vifo ndiyo maafa makubwa zaidi kutokea nchini Indonesia ambayo yamesababishwa na majanga ya asili, tangu janga la Tetemeko la ardhi lililosababisha Tsunami na kuuwa zaidi ya watu 2,000.