1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiRwanda

Mafuriko makubwa yamewaua watu 129 nchini Rwanda

4 Mei 2023

Mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa yamewauwa watu wasiopungua 129 magharibi na kaskazini mwa Rwanda.

Maafa ya mafuriko nchini Rwanda
Maafa ya mafuriko nchini Rwanda Picha: JEAN BIZIMANA/REUTERS

Kulingana na ripoti ya shirika la utangazaji habari la Rwanda,  idadi ya vifo inazidi kuongezeka.

Mvua kubwa ilianza kunyesha wiki iliyopita na kusababisha mafuriko na maporomoko ya udongo yaliyosomba nyumba kadhaa kote nchini na kuharibu baadhi ya barabara.

Idara ya utabiri wa hali ya hewa ya Rwanda imetahadharisha kwamba mvua nyingi bado zinatarajiwa.

Baadhi ya nchi za kanda ya Afrika Mashariki ikiwemo kusini magharibi mwa Uganda, pia zinakumbwa na mvua kubwa.

Wiki iliyopita, watu wasiopungua watatu walikufa maji baada ya kusombwa na mafuriko katika Kijiji cha Rukungiri Uganda.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW