1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiMalaysia

Mafuriko Malaysia yawalazimisha maelfu ya watu kuhama

21 Desemba 2022

Watu wawili wamefariki na wengine wapatao 72,000 wamelazimika kuyahama makazi yao katika miji mbalimbali nchini Malaysia kufutia mvua kubwa iliyosababisha mafuriko.

Malaysia Überflutung
Picha: Vincent Thian/AP/picture alliance

Majimbo matano yamekumbwa na mafuriko hayo wiki hii, huku serikali ya Malaysia ikiandaa mamia ya sehemu za hifadhi wakati ambapo idadi ya waliolazimika kuyahama makazi yao ikiongezeka.

Mamlaka nchini humo zimetahadharisha kuhusu kutokea mafuriko zaidi katika siku zijazo na kuwataka wakazi kuondoka ikiwezekana.

Wataalam wamesema ukuaji wa haraka wa miji na uharibifu wa misitu imelifanya eneo hilo ikiwa ni pamoja na mjii mkuu Kuala Lumpur kukabiliwa na mafuriko makubwa kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW