1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mafuriko ya ghafla yauwa watu 21 Moroko

15 Desemba 2025

Mafuriko ya makubwa yaliyotokana na mvua kubwa na ya ghafla yameuawa watu 21 katika mji wa pwani ya Moroko wa Safi.

Sehemu ya mji wa pwani wa Safi nchini Moroko.
Sehemu ya mji wa pwani wa Safi nchini Moroko.Picha: Michael Runkel/robertharding/picture alliance

Picha zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zinaonesha maji yaliyochanganyika na matope yakizikokozowa gari na takataka kwenye mitaa ya mji huo ulio umbali wa kilomita 300 kusini mwa mji mkuu, Rabat.

Mamlaka zinasema nyumba zipatazo 70 kwenye mji huo wa kihistoria zimeharibiwa vibaya. Watu wengine 32 wamejeruhiwa na kukimbizwa hospitalini.

Wafuma mazulia wanawake wa Morocco

02:42

This browser does not support the video element.

Wafanyakazi wa uokozi wanaendelea kuwasaka manusura, huku mamlaka za utabiri wa hali hewa zikitangaza kwamba mvua kubwa zaidi inatazamiwa kesho Jumanne.

Kwa mwaka wa saba mfululizo, taifa hilola kaskazini mwa Afrika limekuwa likikabiliwa na ukame, mafuriko na hali mbaya ya hewa mara kwa mara.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW