1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mafuriko ya Sudan Kusini yawaathiri watu milioni 1.4

9 Novemba 2024

Umoja wa Mataifa umesema mafuriko makubwa Sudan Kusini yamewaathiri watu milioni 1.4 huku wengine zaidi ya 379,000 wakipoteza makaazi yao.

Mafuriko ya Sudan Kusini yawaathiri watu milioni 1.4
Mafuriko ya Sudan Kusini yawaathiri watu milioni 1.4 na kuwakosesha makaazi wengine 379,000Picha: El Tayeb Siddig/REUTERS

Afisa wa shirika la kuratibu misaada ya kiutu la Umoja wa Mataifa, OCHA, amesema watu waliathirika wako katika kaunti 43 na katika eneo linalozozaniwa la Abyei ambalo Sudan na Sudan Kusini wanadai kulimiliki. 

Umoja huo pia umeonya juu ya ongezeko la ugonjwa wa Malaria ambao tayari umeanza kuripotiwa katika vijiji kadhaa na kuanza kuupa changamoto mfumo wa afya na kufanya hali kuwa mbaya zaidi katika maeneo ya mafuriko. 

Sudan hali ni mbaya na hakuna ishara ya vita kumalizika

Mashirika ya kutoa misaada yamesema nchi hiyo imeathiriwa pakubwa na mabadiliko ya tabia nchi na huenda ikakabiliwa na mafuriko mabaya kuwahi kushuhudiwa kwa miongo kadhaa hasa upande wa kaskazini.