1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mafuriko yaathiri watu milioni 1.4 Sudan Kusini

9 Novemba 2024

Umoja wa Mataifa umesema mafuriko makubwa Sudan Kusini yamewaathiri watu milioni 1.4 huku wengine zaidi ya 379,000 wakipoteza makaazi yao.

Mafuriko ya Sudan Kusini.
Mafuriko ya Sudan Kusini.Picha: Simon Maina/AFP/Getty Images

Afisa wa shirika la kuratibu misaada ya kiutu la Umoja wa Mataifa (OCHA) amesema watu waliathirika wako katika kaunti 43 na katika eneo linalozozaniwa la Abyei ambalo Sudan na Sudan Kusini wanadai kulimiliki. 

Umoja huo pia umeonya juu ya ongezeko la ugonjwa wa Malaria ambao tayari umeanza kuripotiwa katika vijiji kadhaa na kuanza kuupa changamoto mfumo wa afya na kufanya hali kuwa mbaya zaidi katika maeneo ya mafuriko. 

Mashirika ya kutoa misaada yamesema nchi hiyo imeathiriwa pakubwa na mabadiliko ya tabia nchi na huenda ikakabiliwa na mafuriko mabaya kuwahi kushuhudiwa kwa miongo kadhaa hasa upande wa kaskazini.