Mafuriko yakwamisha watalii karibu 100 Maasai Mara
2 Mei 2024Matangazo
Afisa mwandamizi katika kaunti ndogo ya Narok Magharibi, Stephen Nakola ameliambia shirika la habari la Ufaransa, AFP kwamba takriban watalii 100 au zaidi wamekwama katika nyumba za kulala wageni na maeneo ya kuweka kambi ya mbugani.
Hali ilivyo imesababisha pia ugumu wa kuzifikia baadhi ya kambi. Maasai Mara maarufu duniani, iliyo kusini-magharibi mwa Kenya, ni kivutio cha watalii na makazi ya wanyamapori asilia wakiwemo wale wanaojulikana kama "Big Five", simba, tembo, vifaru, chui na nyati pamoja na twiga, viboko na duma.