Mafuriko yameathiri mamilioni ya watu
5 Agosti 2007Matangazo
Takriban watu milioni 10 wamepoteza makazi yao.Mashirika yanayoshughulikia maafa hayo yamesema,maeneo yaliyoathirika vibaya zaidi ni Kaskazini ya India,Bangladesh na Nepal. Maafisa serikalini wamesema,nchini India peke yake,idadi ya watu waliopoteza maisha katika mafuriko hayo,imefikia 1,100.
Msimu wa mvua za masika huanza mwezi Juni na huendelea hadi Septemba na husababisha mafuriko makubwa,kusini mwa bara la Asia,lakini mafuriko kama ya safari hii,hayakuwahi kushuhudiwa.
Kwa mujibu wa mashirika yanayotoa misaada,kuna uhaba wa maji safi ya kunywa na watu wengi wanateseka kutokana na magonjwa yanayosababishwa na mafuriko kama vile homa ya matumbo na kipindupindu.