1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Janga

Mafuriko yasababisha vifo vya zaidi ya watu 50 Afghanistan

18 Mei 2024

Mvua kubwa inayoendelea kunyeshsha Afghanistan imesababisha madhara maubwa wakati taifa hilo likiwa bado linakabiliana na madhara ya majanga yaliyosababisshwa na mafuriko wiki iliyopita.

Mafuriko Afghanistan
Watu wakionekana nje ya nyumba zilizoharibiwa vibaya kufuatia mafuriko AfghanistanPicha: AP/picture alliance

Maelfu ya majumba yaliharibiwa vibaya huku maeneo makubwa ya mashamba ya watu yakijaa maji. Polisi imesema watu 50 wamekufa baada ya kusombwa na maji yaliyosababishwa na mvua kubwa ya masika katika eneo la Ghor. 

Msemaji wa polisi huko aliyetambuloiwa kama Abdul Rahman Badri amesema watu wengine wengi hawajulikani waliko huku mkuu wa kitengo cha mawasiliano nchini Afghanistan akisema hakuna data zinazoonyesha ni watu wangapi haswa waliojeruhiwa katika dhoruba iliyotokea jana jioni. 

Misaada yashindwa kufikishwa maeneo ya mafuriko Afghanistan

Shirika la chakula duniani limesema waathiriwa wameachwa bila makaazi, mashamba na bila kuwa na namna yoyote ya kujikimu kimaisha.