Mafuriko yaua zaidi ya watu 800 nchini Pakistan.
31 Julai 2010Idadi ya waliofariki kutokana na mafuriko mabaya zaidi katika kipindi cha miaka 80 kaskazini magharibi mwa Pakistan, imeongezeka hadi 830. Umoja wa Mataifa umesema kiasi ya watu milioni moja wameathirika na mafuriko hayo. Takriban madaraja 45 yameharibiwa katika mkoa wa Khyber Pakhtunkhwa pekee. Madaraja hayo pamoja barabara zilizojaa maji yanavuruga jitihada za waokoaji katika jaribio lao la kuwafikia wahanga. Mito iliyofurika kutokana na mvua za msimu wa masika imefunika vijiji na kusomba miundo mbinu ya mawasiliano.
Umoja wa Mataifa umeahidi kutoa msaada wa kibinadamu kwa wahanga. Serikali ya Ujerumani imetoa Euro nusu milioni kama msaada wa dharura. Marekani inatuma helikopta kadhaa zisaidie katika juhudi za uokozi.
Mwandishi, Peter Moss/Reuters/AFP
Mhariri, Mohamed Dahman