1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaAsia

Mafuriko yauwa watu 7 Indonesia wengine hawajulikani walipo

Hawa Bihoga
25 Agosti 2024

Watu 13 wameuwawa na wengine hawajulikani walipo kwenye jimbo la Maluku Kaskazini mwa Indonesia baada ya mafuriko makubwa kulikumba eneo la mashariki mwa visiwa hivyo.

Indonesia | Uharibifu wa miundombinu kutokana na mafuriko.
Picha ya angani ikionesha uharibifu mkubwa kufuatia mafuriko IndonesiaPicha: Adi Prima/Andalou/picture alliance

Shirika la utafutaji na uokoaji la Indonesia Basarnas lilisema kwamba mvua kubwa ilionyesha tangu jana Jumamosi ilisababisha mafuriko makubwa katika kisiwa cha Ternate na kwamba kikosi cha uokoaji bado kinaendeleza juhudi za kuwaondoa waathiriwa.

Vyombo vya habari nchini humo viliripoti kwamba watu 11 wamefariki kufuatia mkasa huo lakini afisa wa shirika la Basarnas hakuthibitisha idadi hiyo ya vifo. 

Soma pia:Idadi ya vifo Pakistan kufuatia mafuriko yapindukia 200

Itakumbukwa kuwa mnamo mwezi Mei takriban watu 60 waliuwawa kutokana na mafuriko na maporomoko ya matope katika mkoa wa Sumatra magharibi mwa Indonesia.