Mafuta ya E10 yazua mjadala Ujerumani
20 Agosti 2012Tuanze na suala la matufa ya kuendeshea magari hapa Ujerumani. Gazeti la Dersdner Neueste Nachrichten linaandika.
"Katika mapambano dhidi ya njaa duniani , wazo la waziri wa ushirikiano wa maendeleo, Dirk Niebels, kwa bahati mbaya halitasaidia, hususan kwa kipindi kifupi kijacho. Sio tu kwamba hadi sasa hakuna mtu anayetumia mafuta hayo. Ni kwa sababu kwa Ujerumani mafuta hayo yanakuwa ni yale ambayo yametumika katika kupikia na hayafai tena hata kuoka mikate. Kuyaweka mafuta haya katika kiwango kimoja na mafuta ya kuendeshea magari ambayo hapa Ujerumani yamepewa jina la E 10, haisaidii kitu. Viwanda vya nishati inayotokana na mbegu za mafuta vitatengenezwa na kilimo kwa ajili ya chakula pia kitafanyika. Hapa si tu kwamba matumizi ya mafuta haya kwa ajili ya kuendeshea magari yataweza kuchunguzwa, lakini pia hali yote ya jumla ya mambo hayo. Kwa sababu kwa kila lita ya mafuta yanayotumika sasa ya Super ama super plus- kuna asilimia tano ya mafuta ya mimea. Matumizi ya sasa ya mafuta haya ya E10 ni hatua ya mwanzo tu."
Gazeti la Stuttgarter Nachrichten kuhusu mada hiyo linaandika.
"Nielbel anatoa tu suluhisho nusu nusu tu kwa mapambano dhidi ya njaa hapa duniani. Kwa kuwa chama chake cha FDP kina fursa katika serikali kutoa uwezekano wa kubadilisha mwelekeo. Kwa kulinda mazingira , kwa kuchukua hatua madhubuti, itawezekana kuzuwia vipindi virefu vya ukame kama ilivyo sasa nchini Marekani ama India. Lakini badala yake mwanasiasa huyo anajaribu kudhibiti mzozo wa chakula kwa kuanzisha siasa zitakazomletea umaarufu wa muda mfupi."
Suala la mwanzishi wa tovuti ya Wikileaks, Julian Assange, pia limezungumziwa na wahariri wa magazeti ya Ujerumani. Gazeti la Donaukurier linaandika.
"Assange na Wikileaks wanataka kuwa katika hali ya kawaida kwa kuweka wazi kila kitu ambacho kina mhuri wa siri. Katika kukimbia kwake kuna kitu ambacho anapaswa kukibeba katika kashfa hii. Kwa kuwa Assange anataka kuzuwia uwezekano wa kuwa mhalifu kwa kutoa fursa ya elimu , lakini sasa anabaki kuwa mpweke na kuharibu nafasi yake pamoja na suala zima alilolianzisha, na uwezekano wa kesi yake nchini Marekani. Assange hahitaji hifadhi ya kisiasa , badala yake awe tayari zaidi kuwajibika."
Kuhusu kujihusisha kwa idara ya ujasusi kuwapatia taarifa waasi nchini Syria , gazeti la Kölner Stadt-Anzeiger linaandika.
"Kuna umuhimu wa kupata maelezo. Kwa hatua hii ya idara ya ujasusi, wizara ya mambo ya ndani si wazi kuwa inawajibika. Kwa kuwa hapa ofisi ya kansela inawajibika na idara hii ya ujasusi. Ama kwa maelezo mengine, hili ni suala la Bibi Merkel. Anataka kama ambavyo inaonekana kila wakati kuingilia kati nchini Syria? Kama ni hivyo aseme wazi, na aombe idhini ya bunge la Ujerumani , ama asitishe mara moja operesheni hiyo nchini Syria."
Hayo ni baadhi tu ya yale yaliyoandikwa na wahariri wa magazeti ya Ujerumani kwa leo. Aliyewadondolea hayo yote hii leo ni Sekione Kitojo.
Mwandishi: Sekione Kitojo / inlandspresse
Mhariri Othnan Miraji