1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiBurkina Faso

Magaidi kadhaa wauawa Burkina Faso

10 Machi 2023

Jeshi la Burkina Faso limesema limewaua magaidi 112 katika mfululizo wa mapigano hivi karibuni.

Burkina Faso | Soldaten in Ouagadoudou
Picha: Kilaye Bationo/AP Photo/picture alliance

Taarifa iliyotolewa na kamandi ya jeshi imeeleza kuwa operesheni kubwa kadhaa zimeanzishwa kwa wakati mmoja ili kulikomboa eneo la kaskazini mashariki mwa nchi hiyo, bila kusema ni lini haswa zimeanzishwa.

Mbali na kuwaua magaidi hayo, jeshi hilo pia limeharibu au kukamata silaha,  magari na vilipuzi. Jeshi hilo pia limesema wanajeshi wake 11 wameuawa na wengine wanne wamejeruhiwa wakati wa operesheni hiyo, ambayo ilishuhudia wanajeshi wa nchi kavu wakisaidiwa na kikosi cha anga.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya jeshi, vikosi vya serikali tayari vimeanza kuchukua udhibiti wa maeneo kadhaa, na hasa mji wa mashariki wa Partiaga. Makundi ya wapiganaji wa jihadi yaliwaua raia kadhaa mwanzoni mwa mwezi huu wa Machi katika mji huo, ingawa serikali haijatoa idadi rasmi. 

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW