1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Magari zaidi ya 600 ya mizigo yakwama Namanga

Veronica Natalis
26 Julai 2024

Zaidi ya magari 600 ya kusafirisha mizigo yanayovuka kupitia mpaka wa Namanga uliopo Arusha, yameshindwa kuvuka kwenda Kenya kwa siku ya pili sasa, kutokana na mgomo wa mawakala wa forodha na usafirishaji Tanzania.

Tansania Arusha | Mais Transport | Grenze zu Kenia
Picha: Veronica Natalis/DW

Mlolongo wa magari makubwa ya mizigo unashuhudiwa hapa katika mpaka wa Namanga, uliopo wilaya ya Longido,  idadi ya watu wapatao 300 ambao ni mawakala wa usafirishaji wanaonekana katika makundi wakifanya maandamano huku wakipaza sauti za kushughulikiwa kwa madai yao.

Malori kadhaa yamekwama katika mpaka wa Kenya na Tanzania

Pamoja na mambo mengine mawakala hawa wanalalamika kuhusu mlolongo mrefu wa ukaguzi wa mizigo kwa upande wa Tanzania, pamoja na utaratibu wa risiti za kielekroniki yaani EFD ambazo zimekambazo zimekuwa zikileta usumbufu wakati wa kutolewa kwa wafanyabiashara wa mizigo na kwamba utaratibu wa EFD umekuwa ukifanyika mpaka wa Namanga tu na sio mipaka mingine, jambo ambalo mawakala wanasema linakwenda kinyume na taratibu za usafirishaji mizigo.

Utaratibu huu mpya wa forodha unadaiwa kutokidhi matawa ya wafanyabiashara

Malori ya Mahindi yazuiwa Namanga

02:08

This browser does not support the video element.

Utaratibu huu mpya wa forodha ambao umeanzishwa mipakani na unaodaiwa kutekelezwa katika  mpaka mmoja tu wa Namanga kwa sasa, unaelezwa kutokidhi matakwa ya wafanyabiashara wanaosafirisha mizigo kwenda nje ya Tanzania na mpaka sasa bidhaa hasa za vyakula vimeharibika kutokana na mgomo huu unaoendelea.  Robson Masai ni mmoja kati ya Mawakala amesema wamewapoteza wateja wengi kufuatia hali ilivyo.

Malori yaliyobeba mahindi yakwama mpakani Namanga

Mpaka sasa hakuna taarifa yeyote kutoka serikali ya Tanzania kuhusu mgomo huo, huku maofisa wa mamlaka ya mapato TRA wakisema hawapo tayari kuzungumzia hilo. Hata hivyo kikao cha wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kilichofanyika mwezi Juni mwaka huu kiliweka mikakati ya kuendelea kuondoa vikwazo vya usafiri mipakani na kuahidi kunza utekeleza.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW