Magazeti leo yameandika kuhusu jeshi la Ujerumani kuwekwa huko Lebanon na hali ya elimu nchini Ujerumani.
13 Septemba 2006Kuhusu mada ya kuwekwa jeshi la Ujerumani kulinda pwani ya Lebanon , gazeti la Wiesbadener Kurier, linadokeza kuwa hakuna mtu anaweza kudai kuwa, kulikuwa hakuna uwezekano kwa kazi hii ngumu na ya kihistoria kwa ujumbe huu wa jeshi la Ujerumani, Ujerumani isingeweza kukataa.
Hakuna sehemu yoyote duniani yenye matatizo ya kivita kwa hiyo , ambayo serikali ya Ujerumani ilikuwa na sababu nzuri ya kusema hapana ikilinganishwa na matakwa ya jamii ya kimataifa. Ujerumani ingejivua taratibu , kutoka katika heka heka za kisiasa na pengine kijeshi.
Gazeti la Tageszeitung kutoka Berlin , nalo linadokeza kuwa , matatizo yaliyopo sasa ni kwamba , uwekaji wa jeshi la Ujerumani katika mashariki ya kati sio kimsingi suala la kulikataa. Udhibiti wa eneo la majini lenye umuhimu mkubwa katika nchi hiyo kutokana na amri iliyotolewa ni kinyume na sheria za kimataifa na tena hata kijeshi.
Lakini inawezekana kuwa katika pande zinazohusika katika mzozo huo kuna ushahidi wa kutosha wa kushindwa kwa juhudi za kimataifa kupata suluhisho la amani, ili kuweza kuhalalisha hatua kama hii.
Nani ambaye katika mzozo huu wa mashariki ya kati hajikuti katika nafasi ya kutumiwa kama vibaraka, ni vizuri basi, tukajifunza, Linaeleza gazeti la Tageszeitung.
Gazeti la Dresdner Neuesten Nachrichten linaelezea upande mwingine wa suala hilo. Linasema: Wanajeshi hawatekelezi siasa kabisa, iwapo kazi yao haikuambatanishwa na mkakati wa kuleta amani. Na hii ina maana kuwa , katika hali hii tete, Israel ni lazima ihakikishe inakubali kuwapatia Wapalestina taifa lao.
Kuhusiana na mada nyingine iliyoandikwa katika magazeti ya Ujerumani kuhusu hali mbaya ya elimu, gazeti la General Anzeiger la mjini Bonn linasema , ukitupia jicho ripoti ya elimu kwa vijana , OECD inafichua , ni umbali gani Ujerumani miaka mitano baada ya mshtuko wa ripoti ya PISA, inayohusu uwelewa wa wanafunzi darasani imeweza kimataifa kujikuta.
Kinyume chake , Ujerumani inajikuta katika hali ya kitisho cha kuporomoka kwa nafasi yake ya kupata wahitimu wa vyuo vya juu na kupoteza umuhimu wake kiuchumi. Ishara nyingine za kutahadhari zinaonekana wazi.
Utayarishaji mbaya, na upatikanaji wa nafasi za masomo ya juu kama ilivyokuwa hapo zamani ubaguzi kwa wanawake na kutobadilika kwa uhusiano kati ya asili ya mtu na mafanikio, yanabaki kuwa mbele katika orodha ya matatizo kadha yanayoikabili nchi hii.
Gazeti la Mainz – Allgemeine Zeitung linatafuta njia za kutoka katika matatizo haya na kubaki hapo:
Linasema: Kuwashirikisha wazazi ni vizuri na muhimu, hawawezi lakini kuamua peke yao hatima ya kielimu ya watoto wao. Elimu ni jukumu la shule. Ndio sababu basi ni muhimu , kutokana na kupungua kwa fedha za elimu , kujaribu kuwekeza fedha zaidi ili kupata elimu bora.
Na gazeti la Offenburger Tageblatt linahitimisha kwa kusema kuwa kila mmoja wetu ni lazima achangie, ili Ujerumani ijikute tena katika nafasi ya juu ya kielimu.