MAGAZETI YA UJERUMANI YAMECHAMBUA ATHARI ZA UCHAGUZI WA BUNGE LA ULAYA NA PIGO KWA CHAMA-TAWALA CHA SPD
15 Juni 2004GAZETINI: 15-06-04
Tuanze na gazeti la FRÄNKISCHE TAG linalochapishwa huko Bamberg.Gazeti hilo likizungumzia kushiriki kwa wapigakura wachache katika uchaguzi wa bunge la ulaya laandika:
"Kiroja cha mambo ni kuona kushiriki kwa wpaigakura katika chaguzi za Bunge la ulaya kunazidi kupungua wakati huo huo madaraka ya, Umoja wa Ulaya,umesalia kuwa ni Umoja wenye shida ,umefungamana na umangimeza na unatoa sura ya kuleta udhia wa kilaaina."-hilo limekua FRANKISCHE TAG linalochapishwa mjini Bamberg.
Ama BADISCHEN NEUSTEN NACHRICHTEN kutoka mji wa Karlsruhe linahisi kwamba, UU hauna shida katika umuhimu wake, bali una kasoro katika kutothaminiwa kwake.Wakati wa kampeni za uchaguzi wa Bunge la Ulaya wapigakura haraka hugundua kuwa ushawishi wa wanasiasa wa kitaifa takriban mara nyingi unakadiriwa kupita kiasi na ule wa wabunge wa Ulaya, mara nyingi hudharauliwa.Wabunge wa Shirikisho mjini Berlin wanapaswa kwahivyo , kuungama kuwa mara nyingi wanabidi kuwapigia debe wenziwao wa Brussels." Hayo ni maoni ya BADISCHEN NEUESTEN NACHRICHTEN.
Gazeti linalochapishwa mjini Dusseldorf la kibiashara-HANDELSBLATT linahisi limegundua chanzo cha wapigakura kutoonesha shauku na uchaguzi wa Bunge la Ulaya.Laandika:
"Katika mambo mawili muhimu wabunge wa Ulaya wanahisi wamegeuzwa kama watoto wasio na akili ambao wametupwa pembeni.Wamejionea kwa macho yao jinsi gani dola kuu zanachama wa Umoja wa ulaya zilivyoyakiuka yale mapatano ya kuimarisha sarafu ya ya kutunga Katiba ya UU,wamepokonywa madaraka na serikali zenye uwezo wa kuamua hatima ya katiba hiyo. Kwamba Bunge la Ulaya katika m aswali hayo 2 muhimu linavutana si kitu , hata hii ikiongoza katika msukosuko wa taasisi za Umoja wa ulaya."
Gazeti la MÄRKISCHE ALLGEMEINE kutoka Potsdam lachambua:
"Chama cha kijamaa cha Social democratic Party SPD kwa zaidi ya karne moja kimejitembeza kuwa chama kinachowapigania na kuwatetea wanyonge.Katika uwanja huu hadi karibuni kikiwekewa matumaini na wapigakura wake kwamba katika sera zake za mageuzi hakitapunguza matumizi katika mfumo wa kuwasaidia wanyonge.SPD sasa sio chama barabara katika madaraka.."
Ama gazeti la NEUE WESTFÄLISCHE linahisi kwa upande mmoja chama cha SPD chaweza kujifunza kutoka chama cha walinzi wa mazingira cha KIJANI.
Mara kwa mara chama cha KIJANi chadhihirika viongozi wake wanazifahamu vyengine kabisa kuliko wenziwao wa SPD hatua za mageuzi za Agenda 2010.Laiti waakilishi wote wa chama cha SPD bila ya kuregarega wangetetea sera zao kwa wapigakura licha ya taabu zinazoambatana na mageuzi hayo, basi chama hiki leo kingejikuta katika hali bora kuliko ilivyo.
Kuhusu dai la Kanzela Gerhard Schröder kuendelea na sera zake kama alivyofanya hadi sasa,gazeti la DIE WELT laandika:
"Hakuna kinachokwenda pamoja si mpango wa chama wala mkondo wake kinaofuata, si uongozi wala si Kanzela mwenyewe na chama chake.
Licha ya kuithamini kote Agenda 2010,uchumi ungali unazorota,kwani upepo wa kupalilia kufufuka kwake, si mkali.Kwa jicho hili,matamshi ya Schröder tangu kwa ujuzi hata kwa tabia yake ni makali mno.......
Gazeti la STUTTGARTER ZEITUNG kwa upande wake linachambua hivi:
"Schröder na chama chake cha SPD hawana chaguo jengine isipokuwa: wanalazimika kushikilia uzi ule ule na kutarajia hali ya uchumi itaboreka.Muungano wa Upinzani wa CDU/CSU halkadhalika, usingechukua mkondo mwengine isipokua huo huo.Ndio maana ,unashukuru kwamba uchaguzi mkuu haufanyiki kabla 2006. Kwa hali hii waweza kushangiria ushindi."