Magazeti yazungumzia tathmini ya Olimpiki
13 Agosti 2012Mashindano haya ya olimpiki 2012 hayakuwa tu mashindano yenye kusisimua , lakini yamefungamanishwa pamoja na tamasha lililokuwa na ucheshi wa Waingereza na pia kufurahisha macho. Ilikuwa pia michezo iliyoleta utatanishi kati ya binadamu na vifaa vya ufundi na pia kushindwa kufikia viwango wanamichezo vya olimpiki. Kamati ya olimpiki ya Ujerumani pamoja na mashirika ya michezo mbali mbali yametakiwa na wizara ya mambo ya ndani ya Ujerumani kutumia vyema fedha za walipa kodi na kuweza kuleta medali nyingi, kama ilivyofanya Uingereza. Taarifa juu ya tathmini ya ndani ya wadau wa michezo wa timu ya Ujerumani ni kwamba wanamichezo hao wasibadilishwe. Hadi pale yatakapofanyika mashindano kama hayo mjini Rio mwaka 2016 utapatikana ufumbuzi wa hara katika mfumo wa kile kilichokwenda kombo.
Lakini gazeti la Berliner Morgenpost. Likizungumzia kuhusu tathmini ya timu ya Ujerumani katika michezo hii ya Olimpiki linasema.
Mbali ya mwanzo usioridhisha washiriki wa timu ya Ujerumani katika mashindano haya ya Olimpiki hatimaye walifanikiwa kupata medali kadha kuliko ilivyokuwa miaka minne iliyopita kule Beijing, licha ya kuwa mavuno ya medali za dhahabu yamepungua kutoka medali 16 za dhahabu na sasa ni kumi tu. Tunajivunia pamoja na hayo kikosi hiki, kama alivyosema rais wa shirikisho la olimpiki nchini Ujerumani, Thomas Bach, ambaye ametoa tathmini ya kutia moyo kwa timu hiyo.
Mitt Romney mgombea wa kiti cha Urais nchini Marekani amemteua mgombea wake mwenza. Gazeti la Saarbrücker Zeitung likiandika kuhusu mada hiyo linasema.
Kwa kuwa na Paul Ryan mpambano sasa umewadia, na mlingano umetiwa makali. Mitt Romney hakuamua kuwa na mtu wa nadharia za kati kwa kati katika matendo, kwa ajili ya wadhifa huo wa makamu wa rais. Badala yake amemteua mtu ambaye anaimani na nadharia , kama vile alivyoamini Uncle Sam,katika mpango wake wa kijamii , kuwa sehemu ya tatizo ndio sehemu ya jawabu. Vuguvugu la kundi linalojulikana kama Tea Party, limepata mtu wao wanaempenda katika wadhifa huo, ambapo ataweza kumsaidia Romney kuwavuta wanachama wa kundi hilo la nadharia za mrengo wa kulia la chama cha Republican , kundi lenye wanachama milioni kadha , ambalo hadi sasa hajaweza kulivutia sana.
Nalo gazeti la Badische Zeitung kutoka Freiburg likiandika kuhusu mada hiyo linasema.
Kwamba Paul Ryan hana uzoefu katika sera za mambo ya kigeni , hilo halimshughulishi sana Mitt Romney. Sera za mambo ya kigeni mara chache zimechukua nafasi muhimu katika kampeni za uchaguzi huu. Uteuzi huo wa Ryan unazidi kumwelekezea lawama Romney kuwa hajali masuala ya kijamii. Kwa kukubali kujiingiza katika hali hii tete, ni mafanikio katika mkakati wa Barack Obama , ambaye ni mahiri kwa kutoa changamoto kwa mshindani wake katika mijadala ya kampeni.
Na kuhusu hali ya mvutano kati ya Israel na Iran, Gazeti la Hannoversche Allgemeine Zeitung linaandika.
Ehud Barak sasa anatoa aina mbili za ujumbe. Anaiambia jumuiya ya kimataifa : kuwa msituzuwia tena. Na anawaambia Waisrael : Mjilinde , ingieni mafichoni , dunia inapaswa kutambua , kuwa uongozi wa Israel uko tayari kufanya jambo lolote wakati wowote.
Hayo ni baadhi ya maoni ya wahariri wa magazeti ya Ujerumani hii leo kama mlivyokusanyiwa na Sekione Kitojo.
Mwandishi : Sekione Kitojo / Inlandspresse
Mhariri : Abdul-Rahman,Mohammed