Magazetini: Kramp-Karrenbauer na hatimaya yake
22 Julai 2019Tuanze na gazeti la Neue Osnabrueker Zeitung akizungumzia kuhusu wasi wasi katika masuala ya kiusalama katika uandikishaji wanajeshi katika jeshi la Ujerumani. Mhariri anaandika:
"Katika muda wa miaka miwili ni wanajeshi 21 tu ambao walitaka kujiunga na jeshi la Ujerumani waliondolewa kupitia uchunguzi, kwasababu walikuwa ni wenye msimamo mkali wa mrengo wa kulia. Idadi hiyo ndogo ya walioondolewa pamoja na mmoja ambaye alituhumiwa, haiakisi kiwango kilichopo. Tatizo kubwa bado ni kuhusu kile wanajeshi ambao bado wamo katika jeshi wanachokiwakilisha. Waziri wa zamani wa ulinzi Von der Leyen alikosoa tatizo la mitazamo ya wanajeshi. Mrithi wake Annegret Kram-Karrenbauer kwa upande wake anazungumzia kwamba haiwezekani kuwaweka wanajeshi wote kuwa washukiwa. Kwa hilo Kramp-Karrenbauer anajitenga na kosa kubwa la matamshi ya mtangulizi wake."
Gazeti la Reutlinger General-Anzeiger likizungumzia kuhusu jeshi la Ujerumani ameandika:
"Iwapo Kram-Karrnbauer anaweza kweli kuokoa hali ya uaminifu wa jeshi la ulinzi la Ujerumani, hali hiyo inategemea iwapo, anaweza kutoa matamshi sahihi ambayo anaweza kuyafanyia kazi. Wanajeshi watakuwa kiasi na shaka shaka iwapo ataweza kuweka miundo mbinu bora katika jeshi. Iwapo hali hii haitakuwapo, sauti za shutuma haraka zitaanza kuwa kubwa , kwamba anataka kutumia wizara hiyo ya ulinzi kama jiwe la kukanyaka kurukia katika wadhifa wa ukansela."
Mhariri wa gazeti la Frankfurter Allgemeine Zeitung anazungumzia kuhusu suala la Iran kuwa katika mvutano na mataifa ya magharibi. Mhariri ansema tangu pale rais wa Marekani Donald Trump kuiondoa nchi yake katika makubaliano ya kinyuklia, hali ya mashariki ya kati sasa inaonekana hivi : Mhariri anaandika:
"Iran ilichukua hatua za kimapambano zaidi kuelekea mataifa ya Kiarabu, lakini mpango wake wa kinyuklia ulikuwa chini ya udhibiti wa kimataifa. Leo hii Iran inachukua tena hatua za kimapambano zaidi kwa mataifa ya Kiarabu na inajenga upya mpango wake wa kinyuklia, na inavuruga njia muhimu kwa ajili ya uchumi, njia inayopita meli za kibiashara katika mlango bahari wa Hormuz. Mhariri anaandika kwamba hapa ni lazima kupambana. Ujerumani na Ufaransa kwa mara ya kwanza mwishoni mwa juma , zimejiweka upande wa Uingereza. Hii ni hatua nzuri. Kwa wastani Iran inataka sasa kuzigawa nchi za Ulaya. Pamoja na hayo ni lazima tukubali kuwa funguo wa matatizo haya yote uko mikononi mwa Marekani."