Magazetini: Kuimarishwa kwa sheria ya waomba hifadhi
3 Januari 2019Mhariri wa gazeti la Der neue Tag akiandika kuhusu uhalifu huo mjini Amberg na Bottrop anasema kwamba ni hatari na makosa , kwamba mashambulizi yaliyotokea mjini Amberg yanachukuliwa kisiasa zaidi, wakati mtu ambaye ameonesha chuki dhidi ya wageni katika eneo la Essen kuwa ni mtu aliyechukua uamuzi wa pekee na mwenye matatizo ya akili. Kile matukio yote mawili yanachoshabihiana, ni kwamba matukio hayo yamefanywa na wanaume kwa matumizi ya nguvu.
Kila mara ni wanaume. Kwa hiyo kuna maswali mengi muhimu. Vipi jumuiya ya watu wapenda amani wanaweza kudhibiti hali hii ya watu kutaka kufanya uhalifu huu?
Nae mhariri wa gazeti la Berliner Morgenpost akizungumzia mada hiyo anaandika: Waziri wa mambo ya ndani Horst Seehofer amechukua uamuzi mkali dhidi ya kundi la vijana wanne wanaaomba hifadhi ambao walipigana. Lakini baada ya tukio la wafuasi wa siasa kali za mrengo wa kulia mjini Chemnitz Seehofer alitumia zaidi ya wiki moja. Lilipotokea tukio la Amberg lakini alitumia siku tatu. Anatakiwa pia kuweka sawa tukio la shambulio la mjini Bottrop.
Tukio hilo lilifanywa na Mjerumani kutokana na chuki dhidi ya wageni, na kuwagonga watu kwa gari yake akiwalenga watu wenye asili ya kigeni. Matukio yote mawili yanaonesha upana wa ghasia zinazohusiana na matokeo ya mzozo wa wakimbizi wa mwaka 2015. Kile kilicho muhimu zaidi ni utulivu wa kisiasa na kuchukua hatua za usawa na haki. Badala ya kupiga kelele na kuwa mfano wa chama cha AfD, Seehofer na chama cha CSU wanapaswa kuisaidia nchi kufikia malengo sahihi.
Gazeti la Stuttgarter Zeitung, linazungumzia kuhusu miaka 20 ya sarafu ya euro katika mataifa ya Umoja wa Ulaya. Umoja wa sarafu bila kuwa na umoja wa kisiasa hauwezekani, wamewahi kuonya wakosoaji wa sarafu hiyo. Hali ya kutowezekana haipo, kama ilivyoonekana katika miaka 20 iliyopita, lakini kuna ugumu.
Wanasiasa katika mataifa ya Ulaya wanajiuliza maswali mengi na hawajapata muafaka kuhusiana na lengo lao, iwapo kutatokea mzozo mkubwa.
Mzozo wa dunia wa fedha na biashara pamoja na hali ya wasi wasi mkubwa ndani ya kanda ya sarafu ya euro ni matokeo ya hilo. Benki kuu wa Ulaya inajitokeza tu kama jeshi la zima moto.
Nae mhariri wa gazeti la Emder Zeitung akizungumzia kuhusu sarafu hiyo ya euro limeandika: Wengi wa Wajerumani wanataka pia katika enzi hizi za kidigitali kutoachana na sarafu na noti. Hili bila shaka linafahamika. Kwa hiyo huo ni uwezekano tu wa kudhibiti, hali ya kuingia kikamilifu katika utaratibu wa malipo kwa njia za kielektroniki unapaswa kufanyiwa tafakuri.
Mwandishi: Sekione Kitojo / inlandspresse
Mhariri: Idd Ssessanga