Magazeti: kutano wa mazingira wa Umoja wa Mataifa waanza
4 Desemba 2018
Tukianza na gazeti la Badische Neueste Nachrichten la mjini Karlsruhe mhariri anazungumzia kuhusu mkutano wa mazingira , mhariri anaandika:
Ilikuwa ni tone tu katika bahari la fadhaa, wakati Marekani chini ya rais wao Donald Trump ambaye ana shaka shaka na suala la mabadiliko ya tabia nchi , alipoamua kujitoa katika kufanyakazi kwa pamoja na jamii ya kimataifa kuokoa sayari yetu ya dunia dhidi ya uchafuzi wa mazingira. Mtu alifarijika kwamba mataifa mengine kutokana na hali hiyo yanaweza kufanyakazi kwa pamoja. Muungano wa wenye busara utazungumza kwa sauti moja na uungwaji mkono dhaifu wa wale ambao wanaharibu mazingira na wasiojielewa, wangeondolewa itakapofika katikati ya mwaka 2017. Kwa bahati mbaya hayo yalikuwa ni matumaini ya kupindukia, kama inavyoonekana hii leo.
Ni lazima mkutano huu ulete kitu muhimu, na kuondoka katika hali ya kuhodhi na kujisikia vizuri, na kuendelea na mambo mengine , kwa kuwanunua wengine. Anaandika hivyo mhariri wa gazeti la Allgemeine Zeitung la mjini Mainz kuhusu mkutano huo wa mabadiliko ya tabia nchi. Mhariri anaendelea:
Kwa ukweli kabisa , mtu anaweza kusema , hii inaweza kwenda kombo. Kwasababu kimsingi ongezeko la ujoto hususan lina ncha nyingi. Mbali na uzalishaji mkubwa kutoka mataifa yenye viwanda , lakini pia kuna suala la ongezeko kubwa la binadamu.
Gazeti la Suedwest Presse la mjini Ulm linazungumzia kuhusu mada ya vita vya kibiashara kati ya Marekani na China. Mhariri anaandika:
Sio Wajerumani ama Wachina watakuwa wanafurahia matokeo ya muda mfupi sana ya kuepuka vita vya kibiashara vya Marekani ya Donald Trump. Rais huyo wa Marekani atataka kuendeleza mapambano haya, na kila mara atatafuta njia ya kuyaendeleza.
Nalo gazeti la Suedkurie linazungumzia kuhusu vurugu zinazotokea nchini Ufaransa, zinazofanywa na waandamanaji wanaojiita wanaharakati wa vizibao vya njano. Mhariri anaandika:
Magari yaliyochomwa moto pamoja na alama muhimu katika eneo maarufu la mjini Paris la upinde wa ushindi iliyochafuliwa kwa kuchorwa. Mwishoni mwa juma wanaharakati wa vizibao vya njano walionekana katika mitaa mingi ya Ufaransa. Hadi sasa vuguvugu hili limekuwa likipata uungwaji mkono mkubwa. Lakini uharibifu na uchomaji moto mali za watu haujasababisha wanasiasa kuwekwa kikaangoni.
Ndani ya kundi hilo kuna hali ya ongezeko la nguvu , kama iliyotumika katika mkutano wa G20 mjini Hamburg na kuharibu mali za watu. Rais anatumia hali hii ya mabadiliko , anaweza sasa kupambana kuleta utulivu, ambao Wafaransa wanaupenda, wakati wakiona gari inaungua moto nje ya nyumba.
Anatuma polisi katika eneo hilo, na wanaopoteza katika hali hiyo ni wafuasi wa siasa za mrengo wa kushoto nchini Ufaransa. Maandamano ya kijamii hayatayarishwi tena na Wasoshalisti ama Wakomunisti, na hata pia vyama vya wafanyakazi.
Mwandishi: Sekione Kitojo / inlandspresse
Mhariri: Iddi Ssessanga