Magazetini: Siasa za kizalendo barani Ulaya
5 Julai 2018Mhariri wa gazeti la Volksstimme la mjini Magdenburg akizungumzia siasa za kizalendo zinavyoshika kasi barani Ulaya anasema, kwamba sehemu kubwa ya siasa za Ujerumani zinaelekea kuwakashifu majirani zetu wanaojionesha kuwa wanakumbatia siasa za kizalendo: Mhariri anaandika:
"Hususan katika Ulaya mashariki mara nyingi hutupiwa lawama. Hii ni kutokana na mageuzi ya mfumo wa mahakama nchini Poland , suala ambalo limekuwa likiishughulisha kwa muda mrefu Halmashauri ya Umoja wa Ulaya. Hapana mhariri anaandika kwamba Ujerumani haina haki ya kushikilia masuala ya kimaadili na uwajibikaji katika Umoja wa Ulaya. Si haki kwa, wakati ukweli uko wazi kwamba hali inabadilika kuhusu uzalendo nchini Ujerumani na unakandamizwa tu. Kutokana na chama cha AfD na hali isiyoshwari kwa wananchi muungano unaounda serikali umo katika hali ya kutafunana kutokana na sera za uhamiaji, Ulaya imo katika hatari kubwa."
Mhariri wa gazeti la Rheinpfalz la mjini Ludwigshafen akizungumzia kuhusu serikali ya siasa kali za mrengo wa kulia nchini Poland anaadika:
"Inaelekea kule Poland wamesahau , kwamba Umoja wa Ulaya sio tu kwamba una maadili yake, lakini pia ni jamii inayofuata haki. Na inaeleweka pale Umoja wa Ulaya unakemea mwanachama pale msingi wa utawala bora unapokandamizwa kwa kuondoa uhuru wa mahakama. Umoja wa Ulaya haupaswi tena kuunga mkono hali hiyo, na kufanya kila linalowezekana kurejesha hali katika njia yake, ili kutekeleza makubaliano yaliyokwisha fikiwa."
Akizungumzia suala la SPD kujiingiza katika mzozo wa wakimbizi unaoutikisa muungano wa vyama vilivyoko serikalini vya CDU na CSU, mhariri wa gazeti la Mitteldeutsche Zeitung anaandika:
"Hakuna mwananchi ambaye anaweza kuelewa , wakati chama cha SPD kutokana na baadhi ya vituo vya kuwahifadhi kwa muda wahamiaji itavunja muungano unaounda serikali ya Ujerumani. Pia kutokana na matukio machache yanayowahusu wakimbizi SPD kinataka kuelekeza hali hiyo katika masuala ya kiutu zaidi, na kusababisha hatari, kutokana na mbinyo huo.
Chama cha SPD kinapaswa kujiweka mbali na masuala fulani, ambayo waliyaacha mwaka 2015."
Gazeti la Allgemeine Zeitung la mjini Mainz likiandika kuhusu mada hiyo kuhusu chama cha SPD linaandika:
"Chama cha SPD kimekuwa kama mtoto mdogo, ambapo wamekuwa wakichezea mchanga pamoja na dada zake, ambao wanapigana na kisha dada hao wakaanza kujenga karsi la mchanga, sasa nae anaingilia kati kupinga ubora wa kasri hilo."
Mada yetu ya mwisho ni kuhusu uokozi wa vijana waliokwama katika pango nchini Thailand. Mhariri wa gazeti la Hessische Allgemeine la mjini Kassel anaandika kuhusu kisa hicho:
"Dunia inashusha pumzi baada ya kugundulika vijana 12 pamoja na kocha wao katika pango ambamo walipotea , lakini bado vijana hao hawajatoka katika hatari dhidi ya maisha yao. Bado hali ni ya kutisha, kwa kuwa vijana hao wanapaswa sasa kufanya mazowezi wa kupiga mbizi, ili kuweza kuokolewa. Inaweza kuchukua miezi kadhaa, hadi pale watakapoweza kuona mwanga wa nje."
Ni maoni ya wahariri wa magazeti ya Ujerumani , kama mlivyokusanyiwa na Sekione Kitojo.
Mwandishi : Sekione Kitojo / inlandspresse
Mhariri: Iddi Ssessanga