Magazetini: Trump kushitakiwa bungeni
23 Agosti 2018Tukianza na gazeti la Die Rheinpfalz la mjini Ludwigshafen, mhariri anasema pekee suala la Cohen linatosha kumshitaki rais Trump katika baraza la Congress. Mhariri anaandika:
"Chama cha rais Trump cha Republican ambacho kina wingi bungeni kwa sasa, kitataka kufanya mambo ya uadui. Wanahofia kwamba kundi la chama hicho la siasa kali za mrengo wa kulia linalomuunga mkono kwa dhati Trump linapaswa kuendelea kumuunga mkono. Katika demokrasia inayofanya kazi ni lazima uongo wa rais na ufuasi wa woga kuhusu kampeni ya chama chake kuwa mada namba moja. Chama cha Democratic ni lazima kijitahidi kupata wingi, mwanzoni mwa mwaka ujao wa 2019 na kuanza muhula mpya wa baraza la Congress kwa kuwa na wingi wa kutosha ili kuweza kumshitaki bungeni rais. Lakini hata hivyo inahitajika kwa mujibu wa katiba , baraza la Seneti likubali kwa wingi wa theluthi mbili , ili kuweza kumtangaza Trump kuwa ana makosa na kumuondoa kutoka madarakani."
Gazeti la Südwest Presse kuhusu mada hiyo linaandika kwamba Cohen na Manafort pekee hawawezi kufikisha rais wa Marekani katika hali ya kuanguka kutoka madarakani. Mhariri anaandika:
"Lakini wamezusha maporomoko, ambayo kwa njia moja ama nyingine yanaweza kuwa na athari kwa Trump. Kitu muhimu kitakuwa , iwapo chama cha Democratic mwezi Novemba takriban katika baraza moja la bunge kitakuwa na wingi. Wanapaswa kwa hiyo kufanya kila linalowezekana, kumfikisha rais Donald Trump katika hali ya kushitakiwa bungeni."
Kwa sasa hakuna ushahidi wa mazungumzo yaliyofanyika kati ya kampeni ya Trump na Urusi, anaandika mhariri wa gazeti la Frankfurter Rundschau. Kwa hivi sasa rais Trump anashutumiwa kuhusiana na fedha alizotoa ili kumnyamazisha mwanamke aliyekuwa na mahusiano nae kitu ambacho ni kinyume na sheria za fedha za michango kwa ajili ya chama. Mhariri anaandika:
"Katika nchi nyingine hali hiyo ingezusha mzozo katika serikali. Nchini Marekani wafuasi wa Trump wanamshangiria shujaa wao , na chama chao na kutupilia mbali msingi yake. Hatua ya kushitakiwa bungeni kwa hiyo haipo. Iwapo kutakuwa na mabadiliko katika wingi wa wabunge bungeni katika uchaguzi wa bunge mwezi Novemba , suala hilo litakuwa na sura nyingine. Mambo mengi yatahusiana na kazi anayofanya Mueller ambaye ndiye anahusika na uchunguzi wa suala hilo pamoja na Trump binafsi."
Mhariri wa gazeti la Stuttgarter Zeitung anazungumzia kuhusu hali ya ukame iliyolikumba bara la Ulaya katika majira haya ya kiangazi. Mhariri anazungumzia kuhusu uamuzi wa serikali kuwapa msaada wakulima kutokana na ukame. Mhariri anaandika:
"Waziri wa kilimo Kloekner kwa msaada huu wa haraka hapaswi kusita. Hali mbaya ya hewa ya majira ya joto sio moja kwa moja matokeo ya mabadiliko ya tabia nchi, licha ya kwamba idara ya hali ya hewa ya Ujerumani inaliangalia suala hili la joto kali ambalo halikuwa la kawaida tangu mwaka 1881 kwa jicho hilo. Pamoja na hayo lakini hakuna kitakachobadilika, kwamba sekta ya kilimo, kama ilivyo sekta ya utoaji wa nishati ama usafirishaji, zilivyojielekeza kupambana na mabadiliko hayo. Na kutokana na hayo kuna nafasi kubwa kwa jamii na pia kwa wakulima kufaidika."
Mwandishi: Sekione Kitojo / inlandspresse / Deutschland
Mhariri: Iddi Ssessanga