1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Magazetini

6 Novemba 2018

Wahariri wa magazeti katika safu zao za tahariri wanatoa maoni juu ya kustaafishwa kwa aliyekuwa mkuu wa idara ya usalama wa ndani nchini Ujerumani, miongoni mwa mengineyo.

Deutschland Hans-Georg Maaßen, ehemaliger Präsident Bundesamt für Verfassungsschutz
Picha: Imago/Ipon

Hannoversche Allgemeine

Juu ya aliyekuwa mkuu wa idara ya usalama wa ndani Hans-Georg Maaßen aliyestaafishwa mhariri wa gazeti la Hannoversche Allgemeine anasema lawama dhidi ya waziri wa mambo ya ndani Horst Seehofer ambaye hadi hapo jana alikuwa anajaribu kuendelea kumbeba na hata kutaka kumpandisha cheo Hans-Georg Maaßen, sasa zinatoka kila upande.

Bwana Seehofer aliamua kumtimua Maaßen baada ya mkuuu huyo wa zamani wa idara ya usalama kutoa hotuba yake ya kuaga baada ya mambo kushindikana kabisa. Mpaka sasa waziri huyo wa mambo ya ndani bado hajamchagua mtu, wa kumrithi bwana Maaßen. Hata hivyo jambo muhimu ni kutambua iwapo bwana  Maasen anawakilisha viongozi katika idara ya usalama wenye mtazamo kama wake, na iwapo yeye ni mmojawapo tu, hilo litakuwa jambo la kutia wasiwasi mkubwa.

Oberhessische Presse

Mhariri wa gazeti la Oberhessische Presse anasema, juu ya mkuu huyo wa zamani wa idara ya usalama wa ndani kwamba uamuzi, uliotokana na juhudi kubwa, ziliopitishwa na vyama vya SPD na CDU wa kumstaafisha haukumvutia bwana huyo, la sivyo katika hotuba yake ya kuaga asingelichagua maneno ya kumfanya mtu asiwe na njia nyingine ila kumtimua tu. Bwana Maaßen ana mipango mingine. Mhariri ansema mtu hahitaji kuwa mbunifu sana kutambua kwamba mkuu huyo aliyeanguka, anapanga kulipiza kisasi dhidi ya wanasiasa na vyombo vya habari, kwa sauti kubwa kwenye   maonyesho ya vitabu mwaka ujao. Iwapo,atajiunga na chama cha mrengo mkali wa kulia, itajulikana hapo baadae.

Nordwest Zeitung

Mhariri wa gazeti la Nordwest anazungumzia juu ya vikwazo ambavyo Marekani imeiwekea Iran. Mhariri huyo anaunga mkono vikwazo hivyo na anafafanua kwamba Umoja wa Ulaya na Ujerumani ni pande zisizojifunza. Umoja wa Ulaya na serikali ya Ujerumani hazitaki kuachana na mtazamo wao wa kuikumbatia Iran, nchi yenye watawala wenye itikadi kali ya kiislamu. Sababu ni uroho na siasa ya kuipinga Marekani bila ya kuyaangalia mambo vizuri. Ushirikiano wa kiuchumi na Iran hauleti manufaa kwa wale wanaotaka mageuzi na badala yake wanaonufaika ni watawala wenye itikadi kali  ya kiislamu.

Volksstimme

Mhariri wa gazeti la Volksstimme kuhusu  mrithi wa Angela Merkel katika chama cha CDU, anatoa angalizo kwa bwana Friedrich Merz anayepewa nafasi kubwa zaidi ya kumrithi Angela Merkel kama mwenyekiti wa chama cha CDU na anasema anasema tangu kansela Merkel alipotangaza nia ya kuachia ngazi ya uongozi wa chama chake cha CDU watu watatu tayari wamejitokeza kugombea wadhifa wa mwenyekiti wa chama hicho na miongoni mwao anayepewa nafasi kubwa zaidi ya kumrithi Angela Merkel ni Friedrich Merz. Sifa kubwa aliyokuwa nayo ni kwamba anawakilisha kile ambacho wahafidhina wanakitamani. Ni mtu anayewakilisha matumaini ya kukirejesha chama kwenye misingi ya jadi lakini anapaswa kuwa mwangalifu, bila shaka anakumbuka yaliyomfika mjumbe wa chama cha SPD Martin Schulz. Alizimika mara moja baada ya kujenga umaarufu katika uchunguzi wa maoni.

Mwandishi:Zainab Aziz/Deutsche Zeitungen

Mhariri:   Yusuf Saumu  

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW