Magazetini:Uturuki yatangaza tahadhari kutembelea Ujerumani
11 Septemba 2017Tukianza na mada kuhusu hatua iliyochukuliwa na Uturuki kuwatahadharisha raia wake kutoitembea Ujerumani baada ya Ujerumani kutangaza pia tahadhari ya kusafiri kwenda Uturuki , mhariri wa gazeti la Stuttgarter Nachrichten anaandika.
Inashangaza, ni kwa nini kuna kuwa na siasa za kitoto kiasi hiki. Baada ya wizara ya mambo ya kigeni ya Ujerumani kusisitiza tahadhari yake dhidi ya kusafiri kwenda Uturuki, kama katika shule ya chekechea, Uturuki nayo inajibu kwa hatua kama hiyo ya tahadhari kwa raia wake kutembelea Ujerumani. Bila shaka watu wanaweza kubishana, kwamba Ujerumani iko salama kiasi gani, baada ya kile kilichotokea katika eneo la Breitscheid na mauaji ya muasisi wa kundi la chini kwa chini la wasoshalisti wa kizalendo. lakini anaandika mhariri kwamba hatua zinazofuata hazipaswi kuwa kama hizi. Hii inaonesha ni kulipiza kisasi tu ambako ni hakuna maana.
Gazeti la Der Neue Tag la mjini Weiden kuhusu mzozo huo kati ya Ujerumani na Uturuki linaandika:
Kwa tangazo hilo la tahadhari ya Waturuki kusafiri kwenda Ujerumani , mzozo huu umefikia katika hatua ya juu kabisa, ambayo mtu anaweza kusema ni ya kipuuzi, kwasababu hali halisi sivyo ilivyo. Ni vigumu kuelewa , kwanini rais wa Uturuki Erdogan analipiza kisasi kwa njia hii ya kipuuuzi, badala ya kuiachia serikali ya Ujerumani kuchukua hatua nyingine ya uchokozi. badala yake taifa hilo ambalo linataka kujiunga na Umoja wa Ulaya liwekewe masharti magumu . Erdogan anataka kwa kila hali kujiunga na Umoja wa Ulaya , na hapa ni lazima kukaza kamba, ili sio tu Deniz Yuecel aachiwe huru , lakini kukaa kimya hakutaleta chochote dhidi ya Erdogan , lakini pengine akili itamrejea
Kwa upande wa kampeni zinazofanyika hivi sasa nchini Ujerumani kwa ajili ya uchaguzi wa hapo Septemba 24 , gazeti la Sueddeutsche Zeitung la mjini Munich linaandika:
Demokrasia inahitaji ushindani, na iwapo hilo halipatikani , kutazuka chama kingine kipya , ili kukidhi mahitaji hayo, na hilo linalo linaweza kuleta hatari ya siasa za kizalendo, msimamo mkali wa siasa za mrengo wa kulia , pamoja na chuki dhidi ya Uislamu. Hili limetokea baada ya kuingia kwa chama mbadala kwa Ujerumani AfD kunatokana na kushindwa kwa vyama vya kawaida vya upinzani. Chama cha Kijani kilidhani, kwamba ndio chama mbadala pekee, ambacho nguvu yake kubwa iko katika kile inachokiamini. Na chama cha mrengo wa kushoto cha Die Linke kiliamini kwa makosa , kwamba kupingana na hali ya sasa ya siasa , kunaweza kukifanya chama hicho kuhodhi madaraka hapo baadaye.
Mwandishi: Sekione Kitojo / Inlandspresse
Mhariri: Yusuf , Saumu