1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Magdeburg: Maswali yaibuka kuhusu hali ya usalama Ujerumani

23 Desemba 2024

Shambulio kwenye soko la Krismasi eneo la Magdeburg katikati mwa Ujerumani limezua maswali kuhusu hali ya usalama na udhaifu wa idara za kijasusi nchini humo.

Magdeburg | Ujerumani | Soko la Krismasi
Wajerumani wakitoa heshima zao za mwisho nje ya Kanisa la Mtakatifu John karibu na Soko la Krismasi, ambapo gari lilivurumizwa kwenye umati wa watu Ijumaa jioni, eneo la Magdeburg.Picha: Ebrahim Noroozi/AP/picture alliance

Hii ni baada ya kubainika kuwa mamlaka nchini Ujerumani ilikuwa imepokea tahadhari ya mapema kuhusu mshambuliaji huyo.

Watu watano waliuawa, akiwemo mtoto wa miaka tisa, huku watu wengine wapatao 200 wakijeruhiwa baada ya gari kuparamia umati wa watu katika soko la Krismasi la Magdeburg Ijumaa jioni.

Soma pia: Ujerumani yachunguza maonyo kuhusu muuaji wa soko la Krismas 

Mshambuliaji huyo, daktari mwenye umri wa miaka 50 mwenye asili ya Saudi Arabia, na ambaye ameishi Ujerumani kwa karibu miongo miwili na kuwa na kibali cha kudumu cha kuishi Ujerumani, yuko kizuizini akisubiri kufikishwa mahakamani kwa mashtaka ya mauaji, jaribio la mauaji na kusababishia watu majeraha ya mwili.

Wanawake wanne wenye umri wa miaka 45, 52, 67 na 75 pamoja na mvulana mdogo waliuawa. Wachunguzi wamesema mshambuliaji huyo alikuwa pekee yake japo wanaendelea kuchunguza tukio hilo kubaini nia yake.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW