1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MAGDEBURG Mpigaji picha za watoto walio uchi ashtakiwa

29 Juni 2005

Mtuhumiwa mkuu kiongozi wa upigaji picha za watoto wa kike walio uchi, amefikishwa mahamani mjini Magdeburg, Ujerumani. Marcel K, anatuhumiwa kuanzisha mitandao kadhaa katika mtandao wa mawasiliano wa internet, ambayo hutumiwa na wauzaji wa picha hizo, nyengine zikiwa za watoto wachanga walio uchi.

Polisi walimkamata Marcel mwezi Septemba mwaka wa 2003, katika opresheni iliyofanywa ulimwnguni kote, iliyojulikana kwa jina, ´Operation Marcy.´ Habari zilizopatikana katika komputa yake, zilipelekea kugunduliwa kwa wafanyabiashara 26,500 wa picha hizo za watoto katika mataifa 166 duniani.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW