1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Magonjwa yasio ya kuambukiza huchangia asilimia 74 ya vifo

21 Septemba 2022

Shirika la afya Ulimwenguni WHO limesema magonjwa yasioambukiza kama ugonjwa wa moyo, saratani na kisukari, yanachangia asilimia 74 ya vifo duniani

Afghanistan | Coronavirus | Hospital in Kabul
Picha: Rahmat Gul/AP Photo/picture alliance

Ripoti ya shirika hilo la Umoja wa Mataifa inaonyesha kwamba magonjwa haya yasioambukiza, ambayo kwa kawaida yanaweza kuepukika na yanayosababishwa na maisha yasiozingatia afya bora yanasababisha vifo vya watu milioni 41 kila mwaka, ikiwemo watu milioni 17 walio chini ya miaka 70. 

Ripoti hiyo iliyopewa jina la "Nambari zisizojulikana" inasema Magonjwa ya Moyo, saratani, kisukarina magonjwa mengine yanayoathiri mfumo wa kupumua yanasababisha vifo vingi duniani kuliko magonjwa ya kuambukiza.

Akizungumza na waandishi habari mjini Geneva, Bente Mikkelsen Mkuu wa shirika la Afya ulimwenguni upande wa magonjwa yasioyakuambukiza, amesema kila sekunde mbili mtu aliye chini ya miaka 70 anakufa kutokana na magonjwa hayo na cha kusikitisha ni kwamba bajeti ndogo inawekwa ndani ya nchi na kimataifa kushughulikia magonjwa yasioambukiza.

Soma pia:Ukosefu wa Mazoezi wachangia matatizo ya kiafya

Magonjwa hayo sio tu moja ya magonjwa yanayowaua watu wengi duniani lakini pia yana athari kubwa wakati wagonjwa wanapopambana pia na janga la COVID 19.Ripoti hiyo imesema watu wanaougua magonjwa yasioambukiza ikiwemo unene kupita kiasi wapo katika hatari kubwa ya kuwa wagonjwa zaidi na hata kufariki iwapo wataambukizwa kirusi cha corona.   

Uvutaji wa sigara na unwaji wa pombe ni mambo yanayochangia magonjwa yasiyoyakuambukiza

Data zilizopo katika ripoti hiyo zinaonesha namna hali ilivyo na namna ulimwengu ulivyolifumbia macho suala hili. Utafiti uliofanywa katika ripoti hiyo ya kurasa 86 unasema  vifo vitokanavyo na magonjwa hayo hutokeasana katika mataifa masikini na yale yalio na uchumi wa kati na hii inamaanisha, suala hili sio tu linapaswa kuangaliwa kama tatizo la kiafya lakini pia usawa ukimaanisha kuwa watu wengi katika mataifa masikini hawawezi kufikia huduma bora za afya, njia za kuepukana na magonjwa haya na hata  huduma bora iwapo wataathirika.

Wataalamu wa afya wakihudumia mgonjwaPicha: Theo Giacometti/Getty Images

Uvutaji wa sigara, unywaji wa pombe, lishe mbaya, kutofanya mazoezi na uchafuzi wa hewa ni mambo yanayotajwa kuchangia uwepo wa magonjwa hayo yasioambukiza. 

Soma pia:WHO: Ugonjwa wa kisukari waongezeka duniani

Doug Bettcher mshauri mkuu wa Mkurugenzi mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesusamesema zaidi ya vifo milioni moja vinawapata watu ambao hawavuti sigara kwahiyo wale walio karibu na wavutaji pia wapo hatarini ya kupata magonjwa hayo.

Watu wengine milioni nane hufa kutokana na lishe mbaya. Unywaji wa pombe pia unachangia kuharibika kwa maini na kupatikana kwa saratani ya ini inayoua watu milioni 1.7 kila mwaka huku kukaa bila kufanya mazoezi pia kukichangia vifo vya zaidi ya watu laki 8.

Kwa sasa WHO imesema iwapo mataifa mengi yatafuatilia hali na kuweka bajeti kubwa ya kushughulikia magonjwa hayo pamoja na kuhakikisha huduma bora zinapatikana hospitalini itachangia kupunguza vifo hivyo kwa kiwango kikubwa. Watu pia wametakiwa kukumbatia lishe bora na njia nzuri za kuishi ili kuokoa maisha.

WHO: Unene unachangia magonjwa mengi

01:10

This browser does not support the video element.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW