1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Magwiji wabwagwa kura ya maoni ya CCM Zanzibar

21 Julai 2020

Mchakato wa kura za maoni ndani ya CCM, kuwatafuta wagombea wa nafasi za Ubunge na Uwakilishi unaendelea huku baadhi ya mawaziri wa Serikali ya Zanzibar na Muungano wa Tanzania wakiangushwa katika mchakato huo

Sansibar Ali Karume Präsidentschaftskandidat
Picha: Salma Said

Mchakato wa kura za maoni ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuwatafuta wagombea wa nafasi za Ubunge na Uwakilishi unaendelea huku baadhi ya mawaziri wa Serikali ya Zanzibar na waliokuwa mawaziri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiangushwa katika mchakato huo.

Miongoni mwa walioshindwa katika hatua za mwanzo za mchakato wa kura za maoni ni viongozi maarufu na waliokuwa mawaziri, wakiwemo Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale, Mahmoud Thabit Kombo, aliyekuwa waziri wa fedha wa Jamhuri ya Muungano Sada Mkuya Salum, waziri wa sasa wa Sheria na Katiba, Khamis Juma Mwalimu pamoja, aliyekuwa waziri wa kilimo, Rashid Ali Juma.

Wengine ni aliyekuwa mwanasiasa mkongwe na waziri wa muda mrefu katika wizara ya Fedha Zanzibar, Dk Mwinyihaji Makame na wafanyabiashara maarufu na wafadhili wa Chama Cha Mapinduzi, Mohammed Raza na Ibrahim Raza ambao pia ni miongoni mwa wafadhili wa michezo hapa Zanzibar.

Sababu ya kuangushwa kwa mawaziri katika kura ya maoni

Rais wa Zanzibnar, Dk. Ali Mohammed SheinPicha: DW/M. Khelef

Sababu mbali mbali zinatajwa ikiwa pamoja na viongozi hao kujisahau kwenye majimbo yao, na vijana kutaka damu mpya kwenye uongozi na kuachana na wakongwe. Maryam Ahmed Nassor na Salum Abdallah wachambuzi vijana wa siasa wanaelezea baadhi ya sababu hizo.

Soma zaidi: Hussein Mwinyi kuwania urais Zanzibar kwa tiketi ya CCM

Licha ya baadhi ya wagombea kuangushwa katika awamu ya mwanzo ya kura za maoni mchakato huo unaendelea kwa mujibu wa katibu mkuu wa chama hicho huku akisisitiza aliyeshindwa anaweza kuibuka mshindi na kupitishwa baada ya uchunguzi kufanyika kama rushwa na ukiukwaji wa sheria na taratibu za chama hazikukiukwa.

Mwandishi: Salma Said DW Zanzibar

Mhariri: Iddi Ssessanga


 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW