Mahakama DRC yamhukumu Kamerhe kwenda jela miaka 20
20 Juni 2020Vital Kamerhe ni mwanasiasa mwandamizi zaidi kubabiliana na kesi ya rushwa nchini Congo, ambako kuna kiwango cha ulaji rushwa. Jaji Pierrot Bankenge Mvita amesema kuwa kutokana na kila mtu aliyesikilizwa , mahakama imeonelea kuwa kweli ubadhirifu wa fedha za umma zinazofikia kiasi cha dola za Marekani 48,831,148.
Kamerhe anakana kuiba fedha hizo zilizotengwa kwa ajili ya nyumba za serikali chini ya mpango wa rais Felix Tshisekedi wa siku 100 za ujenzi. Kamerhe alimuunga mkono rais Felix Tshisekedi katika kampeni ya uchaguzi ya mwaka 2018 kwa matarajio ya Tshisekedi kumuunga mkono Kamerhe katika uchaguzi wa mwaka 2023.
Mwanasiasa huyo mkongwe mwenye ushawishi mkubwa katika kuunda serikali alikuwapo katika mahakama hiyo ya wazi iliyoketi kwa muda wa masaa matatu akivalia sare ya jela yenye rangi za buluu na njano na pia alivalia barakoa kumlinda dhidi ya virusi vya corona. Kukamatwa kwake hapo Aprili 8 kulileta wimbi la mshituko katika muungano unaounda serikali nchini humo pamoja na taifa lote kwa jumla.
Wiki iliyopita waziri wa sheria alifichua kuwa jaji wa zamani, ambaye alisemekana hapo mwanzo kuwa amefariki kwa ugonjwa wa moyo mwezi uliopita, alikuwa ameuwawa kinyama.