SiasaIndia
Mahakama India yakataa kuhalalisha ndoa za jinsia moja
18 Oktoba 2023Matangazo
Akisoma hukumu yake, Jaji Mkuu D. Y. Chandrachud alisema ni jukumu la bunge kutoa muongozo wa sheria ya ndoa na haki msingi ya ndoa kwa wanandoa wa jinsia moja haijaainishwa na kulindwa na katiba ya India chini ya sheria ya sasa.
Serikali ya Waziri Mkuu Narendra Modi imekuwa ikipinga hatua za kuhalalisha rasmi ndoa za jinsia moja katika kipindi cha miaka mitano tangu mahakama ya juu kabisa ilipofuta sheria zinazopiga marufuku kufanya mapenzi kati ya watu wa jinsia moja za enzi ya ukoloni.