1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Korti kuu Kenya yakataa kuzuia mjadala wa kumng'oa Gachagua

15 Oktoba 2024

Mahakama Kuu nchini Kenya Jumanne ilikataa kuzuwia kura ya wiki katika Baraza la Seneti kuhusu iwapo kumuondoa mamlakani Naibu wa Rais Rigathi Gachagua. WIki iliyopita bunge la taifa lilipiga kura kumg'oa Gachagua.

Naibu wa Rais wa Kenya Rigathi Gachagua
Hali ni mbaya kwa Naibu wa Rais Rigathi wakati njia zote zikionekana kuteleza kwake.Picha: Andrew Kasuku/AP/picture alliance

Mahakama Kuu ya Kenya Jumanne ilikataa ombi la wanasheria wa naibu wa rais la kuzuia Baraza la seneti kuanzisha mjadala wa hoja ya kumng'oa madarakani baada ya bunge kupiga kura ya kumwondoa ofisini wiki iliyopita. 

Jaji Chacha Mwita aliamua kwamba bunge litaruhusiwa kuendelea na jukumu lake la kikatiba na mahakama haitajihusisha katika mchakato huo.

Hoja ya kumng'oa madarakani makamu wa rais Rigathi Gachagua ilipitishwa kwa kura 281-44 katika bunge wiki iliyopita na kupelekwa kwa seneti, ambayo itaanza kusikiliza mashahidi kuanzia Jumatano.

Gachagua anakabiliwa na hoja ya kumng'oa madarakani kutokana na ufisadi na ukiukaji mwingine wa sheria, ikiwa ni pamoja na tuhuma kwamba alisaidia maandamano ya kupinga serikali mnamo Juni. Anakanusha mashtaka yote dhidi yake.

Jaji Chacha Mwita ametupilia mbali hoja za mawakili wa Gachagua kutaka mchakato wa kumfukuza uzuwiwe kujadiliwa bungeni.Picha: Shisia Wasilwa/DW

Hatma ya Gachuaga mikononi mwa maseneta

Kulingana na Katiba ya Kenya, Gachagua ataondolewa moja kwa moja madarakani endapo mabaraua yote mawili yataunga mkono hoja dhidi yake, ingawa Gachagua anaweza kupinga hatua hiyo mahakamani – jambo ambalo amesema atafanya.

Soma pia: Baraza la Seneti Kenya kujadili hoja ya kuondolewa Gachagua

Jaji Mkuu siku ya Jumatatu alikubali kamati ya majaji watatu kusikiliza maombi sita yaliowasilishwa dhidi ya mchakato wa kumng'oa madarakani.

Mjadala kuhusu hatma yake umepita mipaka ya bunge – wafuasi na wapinzani wa hoja hiyo walivutana katika maeneo ya umma wiki iliyopita baada ya muungano wa serikali kuleta hoja hiyo bungeni.

Rais William Ruto hajatoa maoni rasmi kuhusu kumng'oa madarakani naibu wake, lakini amekuwa na rekodi katika siku za mwanzo za urais wake akisema hatamdhihaki makamu wake hadharani, akirejelea uhusiano mgumu aliokuwa nao na mtangulizi wake, Uhuru Kenyatta, wakati wa muhula wao wa pili wa ofisi.

Seneti inahitaji wingi wa theluthi mbili ili kupitisha hoja ya kumng'oa madarakani Gachuagua. Ikiwa itapitishwa, itakuwa ni mara ya kwanza kwa makamu wa rais aliye madarakani kutiwa hatiani nchini Kenya.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW