1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahakama Kenya yaongeza amri ya kuzuia polisi kwenda Haiti

24 Oktoba 2023

Hakimu Enock Mwita amesema kesi iliyowasilishwa na mwanasiasa wa upinzani Ekuru Aukot kuhusiana na suala hilo itasikilizwa mnamo Novemba 9.

Polisi wa Kenya wanatarajiwa kupelekwa Haiti kulinda amani
Polisi wa Kenya wanatarajiwa kupelekwa Haiti kulinda amaniPicha: James Keyi/REUTERS

Mahakama nchini Kenya leo imetowa uwamuzi wa kurefusha amri ya kuizuia serikali ya nchi hiyo kutowapeleka mamia ya maafisa wa polisi nchini Haiti, kupitia mpango unaoungwa mkono na Umoja wa mataifa kwa lengo la kuleta amani katika taifa hilo la visiwa vya Caribbean.

Hakimu Enock Mwita amesema kesi iliyowasilishwa na mwanasiasa wa upinzani Ekuru Aukot kuhusiana na suala hilo itasikilizwa mnamo Novemba 9.

Uamuzi huo wa mahakama unakuja siku moja baada ya Umoja wa Mataifa kuonya kwamba hali ya usalama nchini Haiti, ambapo magenge ya uhalifu yanadhibiti sehemu kubwa ya nchi hiyo, imezidi kuwa mbaya huku uhalifu ukiweka rekodi kwa kufikia viwango vya juu zaidi.

Kujihusisha kwa Kenya katika mpango huo wa kuwapaleka polisi wake nchini Haiti kumetiliwa mashaka na wengi nchini humo, huku wengi wakijiuliza maswali kuhusiana na busara iliyotumika kuidhinisha mpango hatari kama huo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW