1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahakama Kenya inasikiliza kesi dhidi ya kuondolewa Gachagua

22 Oktoba 2024

Mahakama Kuu nchini Kenya inasikiliza kesi iliyowasilishwa na Makamu wa Rais aliyeondolewa Rigathi Gachagua akipinga kura ya baraza la Seneti iliyomuondoa wiki iliyopita.

Kenya | Wabunge wapiga kura kumtimua Makamu wa Rais Rigathi Gachagua
Spika wa Bunge la Kitaifa Moses Wetangula akiwahutubia wabunge wakati wa hoja ya kutimuliwa kwa Naibu Rais Rigathi Gachagua kabla ya kura ya wabunge ndani ya majengo ya Bunge jijini Nairobi, Kenya Oktoba 8, 2024.Picha: Monicah Mwangi/REUTERS

Mahakama siku ya Ijumaa iliamuru mchakato wa kumuondoa Gachagua usitishwe kwanza, dakika chache tu baada ya bunge kumuidhinisha Waziri wa Mambo ya Ndani Kithure Kindiki kuchukua nafasi yake. Gachaguaalienguliwa na Baraza la Seneti Alhamisi iliyopita kufuatia mashitaka matano kati ya 11 yaliyowasilishwa dhidi yake, ikiwemo kuchochea migawanyiko ya kikabila na kuhujumu idara ya mahakama. Hatua ya kumuondoa Gachagua ilidhihirisha msuguano wa wazi kati yake na Rais William Ruto. Gachagua, mwenye umri wa miaka 59, alimtuhumu Rais Ruto akimuita "mwovu" na akadai kuwa kulikuwa na majaribio ya kumuuwa katika siku za nyuma.