1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahakama ya Kongo yauthibitisha ushindi wa Sassou N’Guesso

Saleh Mwanamilongo
29 Machi 2026

Mahakama ya Katiba ya Jamhuri ya Kongo imethibitisha ushindi wa Rais Denis Sassou-N'Guesso katika uchaguzi wa mwezi huu, akipata muhula wa tano kwa zaidi ya asilimia 94 ya kura.

Jamhuri ya Kongo, Brazzaville 2021 | Wafuasi wanaadhimisha kuchaguliwa tena kwa Rais Denis Sassou Nguesso
Katiba inamzuia Sassou Nguesso kugombea tena mwaka 2031, muhula wake wa tano utakapomalizikaPicha: Olivia Acland/REUTERS

Rais wa mahakama hiyo, Auguste Iloki, alitangaza uamuzi huo baada ya kukataa rufaa ya mgombea wa upinzani Uphrem Mafoula aliyekuwa akipinga matokeo ya uchaguzi.

Matokeo ya awali yaliyotolewa Machi 17 yalionyesha tayari kuwa kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 82 alikuwa anaongoza kwa mbali dhidi ya wagombea sita.

Vyama vikuu vya upinzani vilisusia uchaguzi huo, vikidai kuwa haukuwa wa haki, huku Rais Sassou-N'Guesso akiwa mgombea pekee aliyefanya kampeni kote nchini.

Kiongozi huyo ni miongoni mwa marais waliodumu madarakani kwa muda mrefu barani Afrika.

Hata hivyo, Kongo-Brazzaville inakabiliwa na changamoto kubwa za kiuchumi, zikiwemo deni kubwa, ukosefu wa ajira kwa vijana na umaskini uliokithiri. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW