1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Mahakama India yaidhinisha mwisho wa hadhi maalum ya Kashmir

Saleh Mwanamilongo
11 Desemba 2023

Mahakama ya Juu ya India imeidhinisha uamuzi wa kubatilisha hadhi maalum kwa jimbo la Jammu na Kashmir na kutoa agizo la kufanyika uchaguzi katika eneo hilo Septemba 30.

Mahakama imeamuru ufanyike uchaguzi katika eneo la Jammu na Kashmir
Mahakama imeamuru ufanyike uchaguzi katika eneo la Jammu na KashmirPicha: Indranil Mukherjee/AFP

Eneo pekee la India lenye Waislamu wengi la Jammu na Kashmir limezusha uadui kwa zaidi ya miaka 75 kati ya India na nchi jirani ya Pakistan tangu kuzaliwa kwa mataifa hayo mawili mnamo mwaka wa 1947 baada ya kupata uhuru kutoka kwa mkoloni wa Uingereza.

Amri ya pamoja ya jopo la majaji watano ilifuata zaidi maombi kumi na mbili ya kupinga ubatilishaji huo na uamuzi uliofuata wa kuligawa eneo hilo katika sehemu mbili za shirikisho la maeneo yanayosimamiwa ya Jammu na Kashmir, na eneo la Wabuddha la Ladakh.

Mahakama imeamuru ufanyike uchaguzi katika Jammu na Kashmir, ambayo yaliunganishwa na kuwa karibu zaidi na India baada ya hoja ya serikali, ikichukuliwa kulingana na ahadi ya muda mrefu ya Chama cha Bharatiya Janata BJP cha Waziri Narendra Modi.

Uamuzi huo ni changamoto kwa serikali kabla ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa ifikapo Mei. Wapinzani walishikilia kuwa kikao cha eneo bunge pekee wa Jammu na Kashmir ndio unaweza kuamua juu ya hadhi maalum ya eneo la mlima, na kupinga iwapo bunge lilikuwa na uwezo wa kubatilisha.

Kashmir kurejea jimbo la India ?

Waziri Mkuu wa India Nerandra Modi apokenga uamzi wa mahakama ya nchi yakePicha: Tauseef Mustafa/AFP

Mahakama ilisema hadhi maalum ni kifungu cha muda cha katiba ambacho kinaweza kubatilishwa. Iliamuru kuwa Jammu na

Kashmir inapaswa kurejea kuwa jimbo mara fursa itakapotokea haraka iwezekanavyo.

"Kipengee cha 370 kilikuwa mpango wa muda kutokana na hali ya vita katika jimbo," Jaji Mkuu D.Y. Chandrachud alisema,

akimaanisha kifungu cha katiba ya India ambacho kilitoa hadhi maalum baada ya vita vya kwanza vya India na Pakistan katika eneo la Himalaya.

Waziri Mkuu wa India Nerandra Modi aliita hukumu hiyo kuwa ni "mwanga wa matumaini, na ahadi nzuri zaidiya siku zijazo".

"Ni tamko kubwa la matumaini, maendeleo na umoja kwa dada na kaka zetu huko Jammu, Kashmir na Ladakh," Modi

iliandika kwenye mtandao wake wa X, zamani Twitter.

Pakistan yapinga uamzi wa mahakama ya India

Wizara ya mambo ya nje ya Pakistan ilitangaza leo kwamba serikali ya nchi hiyo imetupilia mbali umazi huo wa mahaka kuu ya India na kusema itawasilisha kesi yake kwenye Umoja wa Mataifa.

Kashmir imegawanywa kati ya India na Pakistan tangu majirani hao walipopewa uhuru kutoka kwa utawala wa Uingereza na kugawanywa mnamo 1947.