1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahakama: Vilabu vya Bundesliga kulipia gharama za polisi

14 Januari 2025

Polisi sasa wanaweza kuvilipisha vilabu vya kandanda Ujerumani kugharamia hatua za ziada za usalama kwenye mechi zinazozingatiwa kuwa za kitisho kikubwa.

Ujerumani | Ligi ya Soka ya Ujerumani | Nembo ya DFL
Vlabu vya DFL sasa vitalaazimika kulipia ulinzi wa polisi UjerumaniPicha: David Inderlied/Kirchner-Media/picture alliance

Mahakama ya juu zaidi nchini Ujerumani imetupilia mbali rufaa iliyokatwa na Kitengo Kinachoratibu Ligi Kuu ya Kandanda ya Ujerumani (DFL) dhidi ya sheria ya mji wa Bremen inayotoza vilabu gharama za ziada za ulinzi katika mechi zinazochukuliwa kuwa hatari. Sheria hiyo, iliyopitishwa mwaka 2014, inalenga matukio makubwa ya kibiashara kama mechi za Bundesliga yanayokusanya maelfu ya watu na kuwa na uwezekano wa kuzuka vurugu.

Soma pia: Kipi kilivisibu vilabu vya Ujerumani Mashariki?

DFL, ambayo imekuwa ikipinga sheria hiyo kwa muda mrefu, ilidai kuwa usalama wa umma ni jukumu la serikali na sio la vilabu vya kandanda. Hata hivyo, Mahakama ya Katiba imeamua kuwa sheria hiyo inaendana na katiba ya Ujerumani. Rais wa mahakama hiyo, Stephan Harbarth, alisema lengo la sheria hiyo ni kuhakikisha gharama za ziada za ulinzi zinabebwa na wahusika wanaofaidika moja kwa moja na matukio hayo.

Mchezaji nyota wa Mainz

01:12

This browser does not support the video element.

Baada ya uamuzi huo, wachambuzi wanatarajia kuona iwapo miji mingine ya Ujerumani itafuata mfano wa Bremen. Wadhibiti wa kandanda wameeleza hofu yao kuwa hatua hiyo inaweza kuongeza mzigo mkubwa wa kifedha kwa vilabu na kuathiri usawa wa ushindani wa ligi, hasa ikiwa majimbo mengine yataanza kutekeleza sheria kama hiyo kwa viwango tofauti.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW