Ndoa za mashoga ruksa nchini Marekani kote
26 Juni 2015Hukumu hiyo iliyopitishwa na majaji watano dhidi ya wanne imesema uhakikisho wa katiba wa ulinzi sawa chini ya sheria unamaanisha kuwa majimbo hayawezi kupiga marufuku ndoa za jinsia moja. Kufuatia hukumu hiyo, ndoa za jinsia moja zitakuwa halali katika majimbo yote 50 ya Marekani.
Jaji Anthony Kennedy, akiandika kwa niaba ya mahakama, amesema matumaini ya wapenzi wa jinsia moja wanaopanga kuoana ni kutengwa na kuishi maisha ya upweke, na kutenganishwa na taasisi za moja ya demokrasia za muda mrefu zaidi duniani. "Wanaomba heshima sawa mbele ya sheria. Katiba inawapa haki hiyo," amesema.
Kennedy ambaye hutoa kura ya maamuzi katika kesi katika kesi zenye mvuto mkubwa, aliungwa mkono na wengine wa majaji wanne waliberali wa mahaka hiyo. Kennedy ambaye aliteuliwa na rais Mrepublican Ronald Reagan mwaka 1988, hivi sasa ameandika hukumu zote muhimu nne kuhusu haki za mashoga, ambapo ya kwanza ilikuja mwaka 1996.
"Bila kutambuliwa, utulivu na kutabirika kwa ndoa, watoto wao watateseka na unyanyapa wa kujua kuw afamilia zao haziko sawa na nyingine," aliandika Kennedy. Katika maoni yanayokinzana, jaji mhafidhina Antonin Scalia, alisema uamuzi huo unaonyesha kuwa mahakama hiyo ni tishio kwa Wamarekani.
Jaji mkuu wa Marekani, mhafidhina John Roberts, alisoma muhtasari wa upinzani wake kutokea nje ya chemba la majaji, hii ikiwa mara ya kwanza kwake kufanya hivyo katika kipindi cha miaka 10 aliokaa katika mahakama hiyo. Roberts alisema ingawa zipo hoja za nguvu kisera katika suala la ndoa za jinsia moja, halikuw ajukumu la mahakama hiyo kuyalaazimisha majimbo kubadili sheria zake za ndoa.
Obama, Clinton washerehekea, Republican walaani
Rais Barack Obama, ambaye ni rais wa kwanza alieko madarakani kuunga mkono waziwazi ndoa za jinsia moja, alisifu hukumu hiyo, akisema kwenye mtandao wake wa twitter kuwa siku ya leo ni hatua muhimu katika safari ya kuhakikisha usawa kwa watu wote.
Naye Hillary Clinton, mgombea anaepewa nafasi kubwa kupitishwa na chama Demokratic kuwania urais mwaka 2016, aliandika kwenye mtandao wake wa twitter kuwa "Najivunia kusherehekea ushindi wa usawa wa ndoa." Hadi mwaka 2013, Clinton alisema alikuwa anapinga ndoa za jinsia moja, lakini alibadili mtazamamo wake tangu wakati huo.
Mgombea wa chama cha Republican Mike Hackabee alisema, uamuzi huu wa udanganyifu ni uababe wa mahakama unaokwenda kinyume na katiba." Mgombea mwingine wa Republican Jeb Bush aliongeza kuwa, " nikiongozwa na imani yangum naamini katika ndoa za asili. Naamini mahakama kuu ilipaswa kuyaruhusu majimbo yafanye uamuzi huu.
Ndoa za jinsia moja zilikuwa zinaruhusiwa katika majimbo 36 ya Marekani pamja na Washington DC. Katika jimbo la 37 la Alabama, mahakama iliondoa marufuku dhidi ya ndoa za jinsia moja, lakini mahakama ya rufaa iliwazuwia maafisa wa serikali kutoa leseni kwa wapenzi wa jinsia moja.
Wapinzani wa ndoa hizo wanasema uhalali wake unapaswa kuamuliwa na majimbo yenyewe, na wengine wanasema kuruhusiwa kwa ndoa hizo ni dharau kwa ndoa ya asili kati ya mwanamume na mwanamke, na kwamba Biblia inalaani mahusiano ya jinsia moja.
Hisia juu ya hilo zilikuwa juu wakati wa mjadala mahakamani mwezi April katika kesi hiyo, pale mwandamanaji alipowapigia kelele majaji na kuwambia wataozea jahanam ikiwa watapitisha hukumu kuunga mkono ndoa za jinsia moja.