1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaYemen

Mahakama moja Yemen yawahukumu kifungo wanaharakati wanne

21 Machi 2023

Mahakama moja katika eneo linalodhibitiwa na waasi nchini Yemen imewahukumu kwenda jela wanaharakati wanne kutumikia vifungo kuanzia miezi sita mpaka miaka mitatu.

View of Big Ben Aden, a clock tower built beside Aden harbor
Picha: Fawaz Salman/REUTERS

Wanaharakati hao wanatuhumiwa  kuwakosoa kupitia mitandao ya kijamii, waasi wa Kihouthi wanaoungwa mkono na Iran.

Kwa mujibu wa wakili wao Waddah Qutaish wanaharakati hao walishtakiwa kwa kuchochea vurugu,kuvuruga amani pamoja na kutumia lugha chafu dhidi ya waasi wa kihouthi.

Soma pia:Pande zinazohasimiana Yemen kubadilishana wafungwa

Walikamatwa na kuzuiliwa mjini Sanaa mwezi Desemba na Januari kwa mashataka yaliyotokana na vidio walizochapisha katika mitandao ya kijamii mwaka jana,wakiwakosoa wahouthi kufuatia madai ya kuhusishwa na rushwa na namna wanavyoshughulikia uchumi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW