Waziri wa zamani wa afya nchini DRC aachiwa huru
8 Juni 2023Matangazo
Longondo, ambaye aliongoza wizara ya afya kuanzia mwaka 2019 hadi 2021, alikuwa akishukiwa na Mkaguzi Mkuu wa Fedha (IGF) kwa ubadhirifu wa zaidi ya dola milioni 7 zilizotengwa kupambana na janga hilo. Wakili wa Waziri huyo wa zamani, Hugues Pulusi Eka ameliambia shirika la habari la AFP kuwa mteja wake ameachiwa leo na Mahakama ya rufaa ambayo ilihitimisha kwamba hakukuwa na ushahidi wa kumuweka hatiani Bwana Longondo. Rais Felix Tshisekedi, aliyeingia madarakani Januari mwaka 2019, ameapa kupambana dhidi ya ufisadi katika uongozi wake.