1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSenegal

Mahakama nchini Senegal yaidhinisha hukumu ya Sonko

5 Januari 2024

Mahakama ya Juu nchini Senegal imeidhinisha hukumu iliyosimamishwa kwa miezi sita dhidi ya kiongozi wa upinzani Ousmane Sonko anayezuiwa jela kwa tuhuma za kashfa.

Kiongozi wa upinzani nchini Senegal Ousmane Sonko
Kiongozi wa upinzani wa Senegal Ousmane Sonko alikamatwa Julai 28, 2023, kwa mashtaka tofauti tofauti.Picha: Seyllou/AFP

Hatua hii inaonekana kuhatarisha nafasi yake ya kuwania urais.

Sonko mwenye miaka 49, ambaye aliwasilisha ombi la kugombea katika uchaguzi wa urais mwezi ujao, amekuwa katika mvutano na serikali ambao umedumu kwa zaidi ya miaka miwili, na uliochochea matukio kadhaa ya machafuko.

Mwezi Disemba mwaka jana, serikali ya Senegal ilipiga marufuku mkutano uliopangwa kufanyika kwa ajili ya kumteua kiongozi huyo wa upinzani kugombea katika uchaguzi huo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW