1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahakama Pakistan yakataa kuakhirisha hati ya kumkamata Khan

16 Machi 2023

Mahakama ya nchini Pakistan imekataa kubatilisha hati ya kukamatwa kwa aliyekuwa waziri mkuu wa nchi hiyo Imran Khan.

Pakistan, Lahore | der ehemalige pakistanische Premierminister Imran Khan
Picha: Musa Virk/Twitter/REUTERS

Wakili wa Khan ameeleza hayo wakati mamia ya wafuasi wake wakiweka mkesha kwenye nyumba ya mwanasiasa huyo katika mji wa Lahore. Wafuasi wake walipambana na polisi walipojaribu kumkamata kabla ya mahakama kuamuru kutulizwa kwa muda zoezi la kumtia mbaroni hapo jana.

Polisi Pakistan imeachana na jaribio lake la kumkamata Khan

Khan aliondolewa madarakani baada ya kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye mwaka uliopita na amekuwa akikabiliwa na kesi kadha wa kadha wakati ambapo anaendesha kampeni ya kutaka uchaguzi ufanyike mapema.

Mwanachama mwandamizi wa chama cha Khan amesema mwanasiasa huyo anahitaji kupewa usalama wa uhakika ili kuweza kufika mahakamani.

Pamoja na mambo mengine Khan anatuhumiwa kupokea zawadi na kuziuza alipokuwa madarakani bila ya kutoa taarifa. Hata hivyo amekanusha madai hayo.


 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW