Mahakama Senegal kuamua hatima ya kiongozi wa upinzani
6 Desemba 2023Kwa mujibu wa taarifa ya mahakama ya rufaa, kikao maalum cha kusikiliza kesi hiyo kimepangiwa kufanyika Desemba 12.
Kiongozi huyo wa upinzani aliondolewa kwenye daftari la uchaguzi baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili jela mnamo mwezi Juni baada ya kukutwa na hatia ya kuhusika na upotoshaji vijana kimaadili.
Soma zaidi: Sonko aanza tena mgomo wa kula
Kiongozi wa upinzani Senegal Sonko arejeshwa gerezani baada ya kutibiwa hospitalini
Mwanasiasa huyo amekuwa katikati ya mvutano na serikali kwa kipindi cha zaidi ya miaka miwili hali iliyozusha machafuko mara kadhaa nchini Senegal.
Sonko anadai kesi zinazomuandama zimetengenezwa kwa lengo kumzuia kugombea uchaguzi wa rais,madai ambayo serikali imeyakanusha ikisema haina ushawishi katika mfumo wa mahakama.