Kamanda wa waasi Thomas Kwoyelo ahukumiwa miaka 40 gerezani
25 Oktoba 2024Matangazo
Kamanda huyo, Kwoyelo alipatikana na hatia ya kushiriki katika vitendo vya ukatili dhidi ya raia na uvunjaji wa haki za binadamu wakati wa uasi uliodumu kwa miaka mingi. Hukumu hii ni moja ya juhudi za serikali ya Uganda kuhakikisha haki kwa waathiriwa wa vita vya waasi ambavyo vimesababisha maafa makubwa na kuathiri jamii nyingi nchini. Kwoyelo ni kamanda wa kwanza wa LRA kufikishwa mahakamani nchini Uganda. Kundi laLRA, lililoanzishwa mwaka 1987, linatuhumiwa kwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu, likiwa limeua zaidi ya raia 100,000 na kuwateka nyara maelfu ya watoto.