Mahakama Ujerumani yaelezwa mipango ya njama ya mapinduzi
29 Aprili 2024Matangazo
Imeelezwa kwamba tayari walikuwa wamekamilisha mipango ya kuanzisha muundo wa kijeshi wa taifa kupambana na upinzani wowote dhidi yao.
Wakati wa kusikiliza kesi dhidi ya washukiwa tisa wa vuguvugu la siasa kali za mrengo wa kulia linalojiita "Reichsbürger" waendesha mashtaka wamesema nia ya watuhumiwa kutumia vurugu ilidhihirishwa na mmoja wao Markus L, alivyofyatua risasi dhidi ya polisi wakati wa kumkamata na kumjeruhi polisi mmoja wakati wa makabiliano hayo.
Kesi hii ni ya kwanza kati ya tatu inayowahusu washukiwa 27 wanaotuhumiwa kula njama ya kupindua serikali ya shirikisho ya Ujerumani, iliyotibuliwa na mamlaka mwishoni mwa mwaka 2022.