Mahakama ya Afrika Kusini yakataa rufaa ya familia ya Lungu
17 Septemba 2025
Matangazo
Jana Jumanne, mahakama hiyo ilithibitisha uamuzi wake na kuizuia familia hiyo kukata rufaa kwa misingi kwamba hakuna matarajio ya mahakama ya juu zaidi kubatilisha uamuzi wa mahakama ya chini.
Katika uamuzi wake, mahakama hiyo imesema imeridhika kuwa hakuna sababu za msingi za kutoa ruhusa ya rufaa kwa sababu suala hilo lina maelezo makhsusi na matarajio finyu ya kubatilishwa .
Lungu, ambaye aliongoza Zambia kuanzia mwaka 2015-2021, alifariki dunia mwezi Juni katika hospitali moja nchini Afrika Kusini akiwa na umri wa miaka 68.
Familia yake inataka azikwe Afrika Kusini na pia kumzuia rais wa sasa wa Zambia Hakainde Hichilema kuhudhuria ama pia kuhutubia katika ibada ya mazishi ya serikali.