1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Sheria na HakiAfrika

Tanzania yatakiwa kuruhusu kupingwa matokeo ya urais

Veronica Natalis16 Julai 2020

Mahakama ya haki za binadamu ya Afrika imeitaka serikali ya Tanzania kurekebisha baadhi ya vipengele vya katiba ya taifa hilo vinavyozuia matokeo ya urais kupingwa mahakamani, kufuatia kesi iliofunguliwa na mwanasheria.

Tansania African Court of Human and people's Rights
Picha: DW/N. Natalis

Baada ya uamuzi wa mahakama hiyo, baadhi ya wachambuzi wa haki za binadamu wanasema kuna mashaka ya utekelezwaji wa agizo hilo kwa kuwa Tanzania ilishatangaza kujitoa katika mahakama hiyo inayoshughulika na haki za binadamu.

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ibara ya 41 kifungu kidogo cha saba kinaeleza kuwa baada ya matokea ya rais yaliyotokana na uchaguzi mkuu kutangazwa na tume ya uchaguzi, matokeo hayo hayawezi kuhojiwa mahakamani.

Msimamohuo unakiuka ibara ya pili na ya saba kifungu kidogo cha kwanza cha mahakama ya haki ya Afrika, ambacho kinaeleza kuwa endapo mtu hataridhika na matokeo hayo ya urais, anahaki ya kukata rufaa.

Kesi hiyo ilifunguliwa na wakili Jebra Kambole wa Tanzania akitaka vifungu hivyo vilivyopo katika katiba vibadilishwe kwani vinakiuka haki za kisheria za binadamu.

Mwanadishi wa DW Veronica Natalis akizungumza na rais wa mahakama ya haki za binadamu na watu ya Afrika Jaji Slyvan Ore, mjini Arusha, Tanzania.Picha: DW/N. Natalis

Utekelezwaji wa hukumu ya mahakama

Tanzania ni miongoni mwa nchi nne zilizotangaza kujitoa katika mahakama hiyo, nchi zingine ni Rwanda, Benin na Cote d'lvoire iliyotoa maamuzi hayo mwishoni mwa mwezi Mei mwaka huu.

Hata hivyo mahakama hiyo inasema kujiondoa kwa nchi hizo katika mahakama ya Afrika hakuzuii nchi hizo kutekeleza na kulinda haki za binadamu.

Dr. Robert Eno, msajili wa mahakama ya Afrika na haki za binadamu, anasema nchi zote nne zilizojitoa zimeeleza wajibu wa kulinda hakiza binadamun kuendelea kutekeleza mkataba wa haki za binadamu.

"Nchi tatu kati ya hizo majaji wake ni majaji wa mahakama hii ya haki za binadamu, hata Rais wa mahakama hii anatoka Cod'lvoir, kwahiyo siwezi kusema kwamba wanakimbia majukumu ya kulinda haki za binadamu,” alisema Dr Eno.

Kenya na Malawi ni nchi ambazo hivi karibuni zilipinga matokeo ya urais waliyotangazwa katika nchi zao jambo ambalo watetezi wa haki za binadamu wanasema ni ukuaji wa demokrasia na ulinzi wa haki za binadamu.


 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW