SiasaBotswana
Mahakama ya Bostwana yatupilia mbali ombi la rais wa zamani
13 Januari 2023Matangazo
Mahakama nchini Botswana imetupilia mbali ombi la rais wa zamani, Ian Khama, kutaka waranti wa kukamatwa kwake uondolewe. Waranti huo ulitolewa na hakimu mmoja wa mahakama ya ngazi ya chini mwishoni mwa Desemba baada ya Khama, ambaye amekuwa akiishi Afrika Kusini tangu Novemba 2021, kushindwa kufika mahakamani kujibu mashitaka yaliyowasilishwa dhidi yake mwezi Aprili.
Mashitaka hayo ni pamnoja na umiliki wa bunduki kinyume cha sheria, kupokea mali ya wizi na kuisajili bunduki kwa njia ya uwongo miongoni mwa mengine. Mahakama kuu mjini Gaborone imesema kuwa ombi la Khama halikutimiza masharti ya waranti huo kuondolewa au kucheleweshwa, na kusema pia alishindwa kuthibitisha kwa nini suala hilo linapaswa kushughulikiwa kama la dharura.