1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBrazil

Mahakama ya Brazil yachapisha video dhidi ya Bolsonaro

10 Februari 2024

Mahakama ya Juu ya Brazil imechapisha video iliyomuonyesha rais wa zamani Jair Bolsonaro akiwaamuru mawaziri wake kumsaidia kukiuka mfumo wa uchaguzi, siku moja baada ya polisi kumuhusisha na madai ya kupanga mapinduzi.

Brazil | Rais wa zamani wa Brazil, Jair Bolsonaro
Rais wa zamani wa Brazil, Jair Bolsonaro akizungumza na waandishi wa habari baada ya Polisi kuwasili katika makazi yake kwa ajili ya msako: Brazilia:03.05.2023Picha: Eraldo Peres/AP/picture alliance

Video hiyo ilisababisha Jaji wa Mahakama hiyo ya Juu Justice Alexandre de Morales kuruhusu polisi kupekua kwenye maeneo ya watu wa karibu na Bolsonaro siku ya Alhamisi.

Hatua hiyo ilifuatia madai kwamba walipanga njama ya kumrejesha Bolsonaro madarakani licha ya kufahamu wazi kwamba asingeshinda kwenye uchaguzi wa Oktoba 2022.

Soma pia: Bunge la Brazil lasema Bolsonaro atakiwa kujibu mashitaka

Kwenye kikao hicho cha dakika 90 na mawaziri mnamo Julai 5, 2022, Bolsonaro alizishutumu mamlaka ya uchaguzi, Mahakama ya Juu na taasisi nyingine kwa kula njama ili kumsaidia mpinzani wake Luiz Inacio Lula da Silva kushinda, huku akiwashinikiza mawaziri hao kukubaliana na madai hayo.